KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI ATHUMANI AKIONESHA BUNDUKI AINA YA SMG NA HIRIZI AMBAVYO VINADAIWA KUTUMIWA NA JAMBAZI ALIYEUAWA |
HUYU NDIYE JAMBAZI TULIYEKUWA TUKIMSAKA KWA MUDA MREFU.....OVA!!! |
“PRESS RELEASE”
TAREHE 25. 03. 2013.
WILAYA YA MBEYA- JAMBAZI MMOJA AUAWA
KWA KUPIGWA RISASI AKIWA
NA WENZAKE
KWENYE HARAKATI ZA KUTEKA MAGARI
ENEO LA
MLIMA NYOKA.
·
TAREHE
25.03.2013 SAA 04:00HRS ENEO LA MLIMA NYOKA WILAYA YA MBEYA KULIKUWA NA
MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA POLISI NA MAJAMBAZI WAPATAO WANNE [4]
·
MAJAMBAZI
HAO TAYARI WALIKUWA WAMEWEKA MAWE BARABARANI KWA NIA YA KUTEKA MAGARI ILI
WAFANYE UPORAJI KATIKA ENEO HILOAMBALO LIMEKUWA NA MATUKIO KADHAA YA WATU
KUPORWA MALI ZAO.
·
JESHI
LA POLISI BAADA YA KUPATA HABARI ZA KUTEGWA MAWE, ASKARI WALIFIKA KWA WAKATI
KWA KUWA POLISIWALIKUWA JIRANI NA ENEO HILO NA KUWEKA MTEGO KWA KUWA MAJAMBAZI
HAWAKUWA WAMEONEKANA KWA WAKATI ULE.
·
BAADA
YA MUDA MAJAMBAZI WALIPOONA TAA ZA GARI WALIJITOKEZA TAYARI KUSHAMBULIA LAKINI
KABLA YA HAPO POLISI WALITOA AMRI YA KUJISALIMISHA KINYUME CHAKE WAKAANZA
KUPIGA RISASI OVYO NDIPO MASHAMBULIZI YA POLISI YAKAFANYWA.
·
KATIKA
MAPAMBANO ALIJERUHIWA JAMBAZI MMOJA KWA RISASI KIUNONI NA UBAVUNI KULIA
,ALIPOWAHISHWA HOSPITALI KWA MATIBABU DAKTARI ALIBAINI KUWA AMEKWISHA FARIKI.
·
JAMBAZI
HUYO ALIKUTWA NA SILAHA MOJA SMG NA AB NA NAMBARI NYINGINE ZIKIWA ZIMEFUTWA NA
MAGAZINE YAKE IKIWA NA RISASI ISHIRINI NA MBILI [22] PAMOJA NA MAPANGA MAWILI
[2].
·
ALIPOFANYIWA
UPEKUZI MAUNGONI MWAKE JAMBAZI HUYO ALIKUTWA NA KITAMBULISHO CHA MKAZI CHENYE
NAMBA B.0010453 CHENYE JINA LA EMANUEL
BLASIUS MDENDEMI ALIYEZALIWA MWAKA 1984 ENEO LA MATAMBA WILAYANI
MAKETE-IRINGA.MAKAZI YAKE NI UWEMBA – NJOMBE.
·
JAMBAZI
HUYU AMEBAINIKA KUWA NI MIONGONI MWA MAJAMBAZI WALIOKUWA KWENYE MTANDAO WA
MAJAMBAZI ULIOKAMATWA HIVI KARIBUNI KUHUSIANA NA MATUKIO WALIYOFANYA MIKOA
MBALIMBALI IKIWEMO MBEYA,NJOMBE NA IRINGA.AIDHA AMEBAINIKA KUSHIRIKI
KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA ASKARI
POLISI PC JAFARI WA KITUO CHA MKWAJUNI – CHUNYA TAREHE 06.02.2013.
·
UFUATILIAJI
WA MAJAMBAZI WALIOTOROKA UMEENDELEA KUFANYWA.KAMANDA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA WAHALIFU HAO AZITOE BILA KUCHELEWA KWA JESHI LA POLISI ILI
ZIFANYIWE KAZI.AIDHA KAMANDA ANAENDELEA KUWATAHADHARISHA MAJAMBAZI /WAHALIFU WA
MAKOSA YEYOTE KUACHANA NA UHALIFU KWA KUWA NI BIASHARA ISIYOLIPA/ISIYO NA FAIDA
BADALA YAKE WAFANYE SHUGHULI HALALI KUPATA MAENDELEO AMBAZO FURSA ZAKE NI
NYINGI.
2.0 HALI YA MAANDAMANO YA CHADEMA YALIYOPANGA
KUFANYIKA JIJINI
MBEYA TAREHE 25.03.2013.
·
HALI
NI SALAMA NA HAKUNA DALILI ZOZOTE ZA MAANDAMANO /VURUGU, WANANCHI WAENDELEE NA
SHUGHULI ZAO ZIKIWEMO ZA KIMAENDELEO KAMA KAWAIDA.
·
NAOMBA
KUTUMIA FURSA HII KUWASHUKURU WANANCHI WOTE WA JIJINI MBEYA NA WILAYA ZOTE KWA
KUWA WASIKIVUNA WATULIVU KWA KUWA AMANI,UTULIVUNA USALAMA NDIO NGUZO KUBWA KATIKA
KUPATA MAENDELEO.
·
NAWAPONGEZA
VIONGOZI WA KITAIFA WA SERIKALI/JESHI LA POLISINA WA CHADEMA KWA MAKUBALIANO
WALIYOFIKIA KWA MASLAHI YA TAIFA.
Signed
By
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment