WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKIPEANA MIKONO NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII, KABLA YA KUANZA KWA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATIKA UWANJA WA SOKOINE LEO JIONI |
TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA-MARA |
TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI-MBEYA |
GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII EMANUEL DAUD AKISHANGAA GOLI LILILOFUNGWA NA MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA DK YA 12 |
GOLI LILIPITILIZA NA KUPENYA KWENYE NYAVU NA KUSABABISHA REFARII NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MBEYA KUREKEBISHA NYAVU HIZO KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA MPIRA HAUJAWEKWA KATI |
Add caption |
GOLI LA TATU KWA UPANDE WA KIMONDO BAADA YA MPIRA WA PENALT GOLI LILIFUNGWA NA MCHEZAJI LUKA MPOSHI DK 59 |
WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKISHANGILIA GOLI |
KIPUTE KINAENDELEA UWANJANI |
PATASHIKA KATIKA GOLI LA POLISI JAMII |
NDEREMO NA HOI HOI ZILITAWALA BAADA YA KIPYENGA CHA MWAMUZI KUPILIZWA HUKU KIMONDO FC IKIWA MBELA KWA MABAO 3-1 |
POLISI WALILAZIMIKA KUMTOA NJE YA UWANJA REFARII KUTOKANA NA KUZONGWA NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO |
HOI HOI ZA FURAHA ZINAENDELEA |
MASHABIKI WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE BAADA YA TIMU HIYO KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA |
SHANGWE NA HOI HOI ZINAENDELEA KATIKA DIMBA LA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MKOANI MBEYA |
KOCHA WA TIMU YA POLIS JAMII MADENGE OMAR AKILALAMIKIA UTARATIBU WA UENDESHAJI WA LIGI HIYO |
PONGEZI ZINAENDELEA |
'TUMESHINDA TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEPITIA VIGINNGI NA VIKWAZO VINGI'' AKIONEKANA ANASEMA MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK MINGA |
SHABIKI WA TIMU YA KIMONDO MBEGU MOJA AKIWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU HIYO SH. 200,000 BAADA YA USHINDI |
TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI MKOANI MBEYA LEO IMEJIPATIA TIKETI YA KUCHEZA LIGI KUU BARAA BAADA YA AKUICHABANGA TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA MKOANI MARA BAO 3-1.
MCHEZO HUO WA LIGI YA MABINGWA WA MKOA ILIZIKUTANISHA TIMU HIZO KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINI JIJINI MBEYA IKIWA NI WA MARUDIANO BAADA YA MCHEZO WA AWALI ULIOCHEZWA MKOANI MARA KUTOKA SULUHU YA MABAO 2-2.
TIMU YA KIMONDO ILIANZA KUONA NYOTA NJEMA KATIKA DAKIKA YA 12 YA MCHEZO BAADA YA MSHAMBULIAJI WA TIMU HIYO CHARLES HIZA KUPOKEA PASI KUTOKA KWA JOFREY MLAWA NA KUPIGA SHUTI ILIYOJAA KIMIANI NA KUMUACHA GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII EMANUEL DAUDI AKISHANGAA GOLINI.
BAADA YA GOLI HILO KULIKUWA NA MASHAMBULIZI YA HAPA NA PALE KATIKA GOLI LA POLISI JAMII AMBAPO DAKIKA TANO BAADAYE TIMU YA KIMONDO ILIJIPATIA GOLI LA PILI LILILOFUNGWA KWA KICHWA NA MCHEZAJI COSMAS MWAZEMBE.
BAADA YA KUFUNGWA FOLI HILO TIMU YA POLISI JAMII ILIAMKA KUTOKA USINGIZINI NA KUFANYA MASHAMBULIZI KATIKA GOLI LA KIMONDO AMBAPO MASHAMBULIZI HAYO YALIZAA MATUNDA DAKIKA YA 30 BAADA YA MSHAMBULIAJI WA TIMU YA POLISI JAMII JOSEPHAT ONYANGO KUIPATIA TIMU YAKE BAO LA KUFUTIA MACHOZI.
HADI TIMU ZINAENDA MAPUMZIKO MABAO YALIKUWA NI 2-1, KIPINDI CHA PILI KILIANZA KWA MASHAMBULIZI YA HAPA NA PALE AMBAPO TIMU YA POLISI JAMII ILIONEKANA KUZIDIWA UWEZO NA TIMU YA KIMONDO BAADAA YA MPIRA KUCHEZWA NUSU UWANJA KWA TAKRIBANI DAKIKA 15.
MASHAMBULIZI YA TIMU YA KIMONDO KWA TIMU YA POLISI JAMII YALISABABISHA KUFANYIKA MADHAMBI KATIKA GOLI LA TIMU YA KIMONDO BAADA YA MCHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII KUMCHEZEA FAULO MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA NA HIVYO KUSABABISHA REFARII KUTOA PENALT AMBAPO MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO LUKA MPOSHI ALIFUNGA GOLI LA TATU KATIKA DAKIKA YA 59 YA MCHEZO.
HADI KIPENGA CHA MWISHO KINAPULIZWA KIMONDO ILIKUWA INAONGOZA KWA MABAO 3-1.
KUTOKANA NA MCHEZO HUO TIMU YA KIMONDO IMEJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA AMBAPO TIMU YA POLISI JAMII INATAFUTA NAFASI YA TATU.
Post a Comment
Post a Comment