TAARIFA ZA AWALI ZILISAMBAZWA NA KUTANGAZWA KATIKA MISIKITI MBALIMBALI YA JIJI LA MBEYA IMAMU HUYO ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE MAJIRA YA SAA 7:00 USIKU NA HAKUONEKANA TENA HADI TAARIFA ZINASAMBAZWA MISIKITINI.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZILIZOTANGAZWA MISIKITINI WAKATI WA IBADA YA SWALA YA IJUMAA SHEKHE HUYO ALITOKA NDANI KWA NIA YA KUJISAIDIA LAKINI HAKUREJEA TENA.
MARA BAADA YA TAARIFA ZA KUTOWEKA KWA SHEKHE HUYO WAUMINI WALISAMBAA SEHEMU MBALIMBALI JIJINI HUKU BAADHI YAO WAKIELEKEA MAPORINI PEMBEZONI MWA MJI NA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI ZA JIJINI KUJUA KAMA AMEPATWA NA TATIZO LOLOTE.
AKIZUNGUMZIA NA MWANDISHI WA BLOGU HII MKE WA SHEKHE HUYO BI. HALIMA KALINGA ALISEMA KUWA ALIPATA TAARIFA ZA KUTOWEKA KWA MUMEWE MAJIRA YA SAA 7:00 USIKU NA KWAMBA ALIDHANI KUWA MUMEWE ALIKUWA AMEENDA KUSWALI SWALA YA USIKU TARAWEHE NA AMECHELEWA KURUDI NYUMBANI.
HATA HIVYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA BLOGU HII GHAFLA ILIPIGWA SIMU KWAMBA SHEKHE HUYO AMEONEKANA KATIKA ENEO LA MLIMA NYOKA AMBAKO ALIKUWA AMESHIKA NJIA KUELEKEA USANGU HUKU AKIWA AMESHIKA TOCHI NA BAKORA YAKE.
MARA BAADA YA KUFIKA NYUMBANI SHEKHE HUYO ALIKUWA KATIKA HALI YA UCHOVU AMBAPO ALIPEWA UJI NA KUJIPUMZISHA.
SHEKHE YASIN NGOWI MARA BAADA YA KUREJEA NYUMBANI |
NYUMBANI KWA SHEKHE YASIN NGOWI, GHANA JIJINI MBEYA |
ENEO LA JIJI LA MBEYA LINAVYOONEKANA KUTOKEA NYUMBANI KWA SHEKHE YASIN |
BAADHI YA WATOTO NA WAJUKUU WA SHEKHE YASIN NGOWI WAKIWA WAMEKUSANYIKA NYUMBANI BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KUTOWEKA KWA MZEE WAO |
SHEKHE YASIN MARA BAADA YA KUWASILI MTAANI KUTOKEA MLIMA NYOKA AMBAKO ALIKUTWA NA WASAMARIA WEMA AKIELEKEA USANGU |
Post a Comment
Post a Comment