KIONGOZI
dini ya Kiislamu kutoka msikiti mtakatifu wa Mecca nchini Saudia Shekhe Mohamad
Al-Hazmi amevunja ukimya na kueleza kuwa waislamu wanaojiua au kuua nafsi za
wengine kinyume na haki wanafanya dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Shekhe
Al-Hazmi ambaye anafanya ziara katika mikoa ya Dar es salaam,Mbeya, Iringa,
Arusha na Kilimanjaro alifafanua kuwa ni haramu kwa waislamu kujitoa mhanga kwa
kujiua kwa madai ya kuipigania dini ya Kiislamu.
Akiwa ameambatana
katika ziara hiyo na Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi ya Dhiynureyn Fondation
Shekhe Said Bin Abri,na kutembelea katika msikiti wa Baraa Bin Azb Isanga
jijini Mbeya Shekhe Al-Hazmi alisema hakuna sheria katika uislamu inayoruhusu
mtu kujiua.
Akijibu
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waumini wa msikiti huo baada ya swala ya
tarawehe ambao walitaka kujua iwapo baadhi ya watu wenye itikadi ya dini ya Kiislamu huamua kujiua kwa kujitoa mhanga
kwa madai kuwa wanachokifanya ni kuinusuru dini.
Shekhe
Al-Hazmi alisema kuwa upo mgongano miongoni mwa mashekhe wakubwa juu ya suala
hilo na kwamba hata hivyo ni haramu kwa muislamu yoyote kujiua au kuua nafsi
nyingine na kwamba kitendo hicho sio katika maagizo ya dini ya kiislamu.
Alisema kuwa
katika zama za Mtume Mussa suala la kujiua lilikuwa ni sehemu ya kafara ya
madhambi lakini katika zama hizi ni haramu mtu yoyote kujiua na kwamba kwa
kufanya hivyo anakuwa amemkosea Mwenyezi Mungu.
Shekhe Al
Hazmi ambaye alikuwa akizungumza kwa lugha ya kiarabu kupitia mkalimani Shekhe
Ibrahimu Bombo aliongeza kuwa yapo mazingira katika zama hizi ambapo kuna baadhi
ya watu wanaamua kujitoa mhanga na kwamba suala hilo ni gumu kulielezea kwa
kuwa lina hitilafu kwa mashekhe wakubwa wa kiislamu duniani.
‘’Mazingira
ya jambo hili ni mazito yanahitaji ufafanuzi wa mashekhe, uislamu umezungukwa
na mambo mengi kwa sasa,’’alisema Shekhe Al-Hazmi ambaye ni miongoni mwa
maimamu kutoka katika msikiti mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia.
Hii itasaidia dhana mbaya inayopewa dini ya kiislam
ReplyDelete