TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 14. 08. 2013.
WILAYA YA MBOZI – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 07:00
HRS UKO KIJIJI CHA NANSAMA KATA YA ISANSA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA.
SIJAONA S/O HAONGA MIAKA 45, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NANSAMA ALIKUTWA AKIWA
AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KUTUPWA KATIKA MTO MLOWO NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI MGOGORO WA MASHAMBA KATI YA MAREHEMU
NA SHABANI S/O MBWILI PAMOJA NA MAWAZO S/O MBWILI AMBAO WALITOROKA MARA BAADA
YA TUKIO HILO. MAREHEMU ALIVIZIWA
WAKATI AKIVUA SAMAKI NA PEMBENI YA MWILI WAKE KULIKUTWA
NDOANO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA
MAZISHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHULIA SHERIA MKONONI NA KUITATUA
MIGOGORO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO NA YEYOTE
MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA
CHUNYA – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.08.2013 MAJIRA YA SAA 00:05
HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MARIA D/O MARTIN, MIAKA 37, MNYAMWEZI,
MKULIMA, MKAZI WA KANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI KICHWANI NA KUKABWA SHINGONI
NA MPENZI WAKE AITWAE LAMECK S/O MSANGAWALE, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI
WA KANGA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI
BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MWANAUME MWINGINE. MTUHUMIWA
ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUYATATUA MATATIZO YAO
YA KIJAMII KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA
KUJITOKEZA. PIA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE
NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Imesainiwa
na,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
Post a Comment
Post a Comment