Ads (728x90)


  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13. 06. 2013.


WILAYA YA  CHUNYA  - MAUAJI.
MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 16:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITINDI WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA. HATIBU S/O MWAKALINGA, MIAKA 36, KYUSA, MVUVI, MKAZI WA KIJIJI CHA ITINDI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO MBAVUNI NA WACHUNGAJI NG’OMBE WAFUGAJI WA KISUKUMA. MAREHEMU ALIKUWA NA KUNDI LA SUNGUSUNGU WAKIKAMATA MIFUGO MALI YA WAFUGAJI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA 1. MWANAHELA S/O ? 2.  KABAHUNGU S/O ? NA 3. LUKANGILA  S/O ?.  MIFUGO HIYO ILIKUWA INAKULA MAZAO KATIKA SHAMBA LA MKULIMA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. MIFUGO ILITOROSHWA MARA BAADA YA  TUKIO HILO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI  YA  MWAMBANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.

WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI – AJALI YA  MOTO NA KUSABABISHA VIFO.


MNAMO TAREHE 12.08.2013 MAJIRA YA  SAA 07:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSHEWE KATA YA  UTENGULE USONGWE WILAYA YA  MBEYA VIJIJINI  MKOA WA MBEYA. RAPHAEL S/O MBWIGA,MIAKA 22, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE, AKIWA MNADANI KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KIBIASHARA  ALIPATA TAARIFA ZA KUUNGUA KWA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA VIFO VYA WATOTO WAKE WAWILI 1.DESMOS S/O RAPHAEL,MIAKA 2 NA MIEZI 7,MSAFWA NA 2. DORCAS D/O RAPHAEL, MIEZI 4, MSAFWA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE. CHANZO NI BAADA YA  MAMA MZAZI WA MAREHEMU HAO FLOIZA D/O EMANUEL, MIAKA 20, MSAFWA, MKULIMA,  MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE AMBAYE ALIKUWA AMELALA NA WATOTO WAKE ALITOKA  NJE MAJIRA YA  SAA 06:00HRS KUJISAIDIA NA KUACHA AMEWASHA KIBATARI NA ALIPORUDI ALIKUTA MOTO UNAWAKA NA KUTEKETEZA VYUMBA VIWILI KIKIWEMO WALICHOKUWA WAMELALA WATOTO WAKE. MOTO HUO ULIZIMWA NA MAJIRANI. NYUMBA HIYO ILIKUWA NA VYUMBA VIWILI IMEJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA NYASI. THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOTEKETEA BADO KUJULIKANA. MIILI YA  MAREHEMU IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUZIKWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA MAJANGA YA  MOTO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.


 [ DIWANI ATHUMANI   - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Post a Comment

Post a Comment