Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam limemtia mbaroni askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.
Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipokukutana na waandishi wa habari leo asubuhi alisema kuwa leo majira ya saa 1:30 asubuhi wamefanikiwa kumkamata mtu aliyejitambulisha kwa jina la James Hussen(45) mkazi wa Kimara Tangi Bovu akiwa ndani ya sare za Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani akiwa bize barabarani akikusanya faini kutoka kwa madereva wanaoendesha magari katika njia hiyo.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Kova ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote watoe taarifa Polisi na kwamba mara wanapokamatwa wawatake askari hao kuongozana hadi kituo cha polisi badala ya kukubali kutozwa fini barabrani.

Post a Comment
Post a Comment