MNAMO TAREHE
15.08.2013 MAJIRA YA  SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA BARABARA YA 
MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.765 BBA AINA YA  SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA MBEYA MJINI
KUELEKEA TUNDUMA LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE LILIGONGA  TREKTA AMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA
USAJILI KISHA KULIGONGA GARI ACP 8839
AINA YA  SCANIA  MALI YA 
KAMPUNI YA  USAFIRISHAJI YA  DHANDHO
LILILOKUWA LIKITOKEA TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO
KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU  WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GARI T.765
BBA NA MMOJA NI DEREVA WA TREKTA  AMBAO HAWAJATAMBULIKA
MAJINA WALA MAKAZI YAO,  WOTE WANAUME WALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO.  AIDHA WATU WAWILI  WALIOKUWA KATIKA
GARI ACP 8839 AMBAO PIA HAWAJATAMBULIKA
WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA  KATIKA HOSPITALI
YA  RUFAA MBEYA.  MIILI YA  MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA  SERIKALI VWAWA WILAYA YA  MBOZI. CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)















Post a Comment