MNAMO TAREHE
15.08.2013 MAJIRA YA SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA BARABARA YA
MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.765 BBA AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA MBEYA MJINI
KUELEKEA TUNDUMA LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE LILIGONGA TREKTA AMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA
USAJILI KISHA KULIGONGA GARI ACP 8839
AINA YA SCANIA MALI YA
KAMPUNI YA USAFIRISHAJI YA DHANDHO
LILILOKUWA LIKITOKEA TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO
KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GARI T.765
BBA NA MMOJA NI DEREVA WA TREKTA AMBAO HAWAJATAMBULIKA
MAJINA WALA MAKAZI YAO, WOTE WANAUME WALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO. AIDHA WATU WAWILI WALIOKUWA KATIKA
GARI ACP 8839 AMBAO PIA HAWAJATAMBULIKA
WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA WILAYA YA MBOZI. CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Post a Comment
Post a Comment