Baadhi ya wadau na viongozi wa soka la vijana chini ya miaka 15 wakiwa katika mkutano wa taarifa za kuanza kwa ligi hiyo |
Add caption |
TIMU 6 za soka
la vijana chini ya miaka 15(U-15) zinatarajia kuanza kutimua vumbi katika mchuano
wa ligi hiyo unaozikutanisha timu kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini jijini
Mbeya.
Akizungumzia
ratiba ya mashindano hayo Katibu wa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa
Mbeya(MREFA) Suleiman Haroub alisema kuwa michuano hiyo inazikutanisha timu
sita kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi.
Haroub
alisema michuano hiyo inayoanza leo na kumalizika Septemba 6 itazikutanisha
timu katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza litazikutanisha timu za
Katavi,Njombe na Rukwa, ilhali kundi la pili litazikutanisha timu za Ruvuma, Mbeya
na Iringa.
Wadhamini wa
ligi hiyo kampuni ya Cocacola kwanza imetoa seti sita za jezi na mipira miwili
kwa kila timu.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi seti za jezi kwa viongozi wa timu hizo, Meneja mauzo na
masoko wa kampuni ya Cocacola kwanza kanda ya Mbeya Jayanti Vekarian alisema
kuwa kampuni yake imejitolea kudhamini soka la vijana wa chini ya miaka 15 ili
kuendeleza na kuibua vipaji vya soka nchini.
Vekaria
alisema kuwa kampuni ya Cocacola kwanza iko mbioni kuwapeleka wachezaji nje ya
nchi kwa ajili ya mafunzo zaidi kwa nia ya kuendeleza na kukuza vipaji vya soka
nchini.
Naye mjumbe
wa kamati ya ya maendeleo ya soka la vijana wa (TFF) Daud Yasin alisema kuwa
washindi wa kwanza na wa pili katika michezo hiyo wataenda jijini Dar es salaam
kwa ajili ya kukutana na washindi kutoka kanda zingine.
Post a Comment
Post a Comment