Gari la Polisi maarufu kama Washa Washa ambalo ni mkakati mpya wa Jeshi la Polisi kukabiliana na Uhalifu |
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Rashid Omar akielezea changamoto inazokumbana nazo Jeshi la Polisi nchini katika utendaji wake. |
Katibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya Emanuel Lengwa akifafanua jambo juu ya umuhimu wa Jeshi la Polisi kushirikisha Jamii katika kukabiliana na vitendo vya Uhalifu |
Washiriki wa Mkutano wa siku moja uliolihusisha Viongozi wa Jeshi la Polisi na wadau Jijini Mbeya. |
Washiriki wa mkutano ulioitishwa na Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(hayupo pichani) |
Na Bloga Wetu
JESHI la
polisi limejipanga kutumia njia mpya ya ukamataji salama kwa kutumia maji ya
upupu badala ya kutumia virungu na mkong’oto ili kuwanasa wahalifu wanaokabiliwa na makosa mbalimbali ya
jinai.
Kauli hiyo
imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Rashid Omar alipokuwa
akielezea mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu
katika kikao cha Siku ya Polisi kilichofanyika Jijini Mbeya jana.
Bw. Omar
alisema kuwa jeshi la polisi limejitahidi kwa kila njia kukabiliana na kuzuia
vitendo vya uhalifu ambapo limeamua kutumia njia mpya ya ukamataji salama kwa
kumwagia maji ya upupu badala ya mkong’oto.
‘’Tumeamua
kutumia utaratibu mpya wa ukamataji salama badala ya kupiga sasa tunamwagia
maji ya upupu, njia hii ni nyepesi kwetu kuwanasa wahalifu, hata wakinawa maji
tutawanasa tu, ‘’alisema.
Aidha alisema
Tanzania ni moja ya nchi zinazokabiliwa na ongezeko kubwa la tishio la Uhalifu
na wizi wa kimtandao ambapo ili
kukabiliana na changamoto hizo kuna haja ya kuweka utaratibu wa kuwa na daftari
la wakaazi kwa Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema
utaratibu wa kuwepo kwa daftari la wakaazi utasaidia kuratibu aina ya watu
wanaoishi katika jamii na kwamba matukio ya uhalifu na uvamizi wa Westgate uliotokea
nchini Kenya ni aina ya uvamizi unaopaswa kuchukuliwa tahadhari mapema.
Bw. Rashid Omar alisema kuwa pamoja Jeshi hilo
linachangamoto kubwa katika utendaji wake kutokana na uwiano askari mmoja
kuhudumia raia 1200 ilhali takwimu za Kimataifa ni askari mmoja kuhudumia raia
500.
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alilitaka Jeshi la polisi kuacha
kufanya kazi kwa mazoea kutokana na lawama nyingi zinazoelekezwa kwa jeshi hilo
hususani kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kukithiri kwa vitendo vya
rushwa na ubambikizaji wa kesi.
Alisema kuwa
Jeshi la Polisi linapaswa kufanya kazi kwa weledi na umakini mkubwa hususani
katika kipindi hiki ambacho baadhi ya wananchi wamekuwa hawataki kuheshimu
utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani.
Post a Comment
Post a Comment