Uharibifu na uchomaji wa moto katika vurugu Jijini Mbeya uliharibu miundo mbinu na kuingiza hasara ya sh. milioni 20 |
Kusimama kwa shughuli za Biashara katika vurugu Jijini Mbeya kulisababisha hasara ya sh. bilioni 2.6 |
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara na Viwanda mkoa wa Mbeya TCCIA Julius Kaijage akitoa tathmini ya vurugu za Jiji la Mbeya zilizofanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba. |
VURUGU zilizotokana
na watu wanaodaiwa kuwa ni wafanyabiashara
wa Jiji la Mbeya zilizotokea mwanzoni mwa mwezi huu zimedaiwa kusababisha
hasara ya zaidi ya sh. bilioni 2 ikiwemo uharibifu wa mali za umma, uchomaji wa
barabara na kusimama kwa biashara.
Wakizungumza
katika kikao maalumu kilichohusisha, Jeshi la polisi, wafanyabiashara, wananchi
na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na Mwenyekiti wa
chama cha Wafanyabiashara na viwanda TCCIA Julius Kaijage walisema hasara
iliyotokana na vurugu hizo ni sh. bilioni 2.26.
Mkuu wa mkoa
wa Mbeya Bw. Kandoro alisema kuwa tathmini iliyofanywa baada ya vurugu hizo
kutokea utaigharimu serikali jumla ya sh. milioni 20 fedha ambazo zingeweza
kusaidia huduma zingine za kijamii kama vile elimu na afya.
Alisema kuwa
wananchi wa Jiji la Mbeya wanapaswa kujua kuwa vurugu zozote zinazoambatana na
uharibifu wa mali ya umma hauna tija kwao kwa kuwa unasababisha serikali
kuingia gharama za matengenezo fedha ambazo ni za walipa kodi.
‘’Ifike
mahala wananchi wanapaswa kujua kuwa hasara inayotokea inatugharimu sote, fedha
hizi ni za walipa kodi ambao ni mimi na wewe, tunapofanya uharibifu
tunajirudisha nyuma wenyewe,’’alisema.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa TCCIA Bw.Kaijage alisema kuwa kwa siku mbili ambazo
wafanyabiashara, wamachinga na akina mama Lishe walifunga biashara kutokana na
mgogoro kati yao na Mamlaka ya Mapato TRA umesababisha hasara ya zaidi ya sh
bilioni 2.6.
Alisema ili
kukabiliana na hali ya uvunjifu wa amani unaotokana na watu wanaodaiwa kuwa ni
wafanyabiashara TCCIA imeandaa makubaliano maalumu ya kuunda kamati za ulinzi
katika maeneo ya biashara.
Post a Comment
Post a Comment