TIMU 36 za
kata zinatarajia kuchuana kumtafuta bingwa atakayewakilisha Jiji la Mbeya katika michuano ya kombe la Pepsi Meyors Cup
linalodhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya SBC mkoani Mbeya.
Akizungumza
Jijini Mbeya mratibu wa mashindano hayo Mkurugenzi wa kampuni ya Myway
Entertainment Paul Mganga alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kuchezwa kwa
mtindo wa mtoano kwa awamu ya kwanza kabla ya kuzikutanisha timu 18 ambazo zitacheza
kwa mtindo wa ligi.
Alisema kuwa
mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya vinywaji baridi vya Pepsi
SBC itagawanywa katika makundi 6 ambazo zitajumuisha jumla ya kata 36 katika
viwanja 6.
Mganga
alizitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni Iduda, Uyole, Nsalaga,Igawilo, Iganjo,Itezi,
Ilomba, Mwasanga, Mwakibete,Ilemi, Tembela,Isyesye, Isanga, Itagano, Ruanda,
Mwansekwa, Iyela,Iganzo.
Zingine ni
timu za Mbalizi Road,Sinde,Forest, Mabatini, Sisimba,Maanga, Maendeleo, Iziwa,
Ghana, Nonde, Nsoho, Itiji, Iwambi, Nzovwe, Iyunga, Kalobe na Itende.
Alisema kuwa
mshindi wa kwanza katika ligi hiyo ataondoka na kitita cha sh. milioni 5 ikiwa
ni Bajaj yenye thamani ya sh. milioni 4 pamoja na fedha taslimu sh. milioni 1
ambapo mshindi wa pili ataondoka na sh. milioni 1.5 ilhali mshindi wa tatu
atajinyakulia jumla ya sh. 500,000.
Kwa upande
wake Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga alisema kuwa mashindano hayo
yatasaidia kuibua vipaji kutoka kwa wachezaji wa timu za mitaani ambao watapata
fursa ya kuichezea timu ya ligi kuu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri
ya Jiji la Mbeya.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SBC Jacques Pretorius alisema kuwa kampuni
yake imejitolea kudhamini ligi hiyo kutokana na umuhimu wake wa kurejesha
huduma kwa walaji wa vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBS inayozalisha vinywaji vya Pepsi Jacques Pretorius akielezea mchango wa kampuni hiyo katika masuala ya michezo duniani. |
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakijumuika katika uzinduzi wa ufadhili wa Kampuni ya SBC kudhamini kombe la Meya Jijini Mbeya. |
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Mussa Zungiza akielezea umuhimu wa ufadhili wa Pepsi kwa kombe la Meya Jijini Mbeya. |
Mratibu Mashindano ya Kombe la Meya Paul Mganga kampuni ya Myway akizungumzia utaratibu wa mashindano ya Meya Jijini Mbeya. |
Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga akishukuru udhamini wa kampuni SBC juu ya mashindano ya Meya. |
Mratibu wa mashindano ya Kombe la Meya Paul Mganga akizungumza ratiba ya mashindano. |
Meya wa Jiji la Mbeya akipongezana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBC baada ya kukubali kudhamini mashindano ya kombe la Meya. |
Post a Comment
Post a Comment