Ads (728x90)

Wababe wa Prison kikosi cha JKT Oljoro ambacho kiliwapeleka mchakamchaka Maafande wa Prison na kuwatandika nyumbani Bao 1-0

Kikosi cha Prison kilichocheza na Maafande wa JKT Oljoro na kutandikwa bao 1-0

JKT Oljoro wakifurahia bao lililopatikana dakika ya 6 ya mchezo

Prison inapaswa kujilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi ambapo katika dakika ya 21 mchezaji wa timu ya JKT  Nurdin Mohamed alimfanyia madhambi mchezaji wa Prison Six Ali katika eneo la adhabu na hivyo mwamuzi wa mchezo huo Zakaria Jacob kutoka Pwani alilazimika kutoa penati kwa Prison.


Hata hivyo penati hiyo iliyopigwa na mchezaji wa Prison Jeremia Juma iliokolewa na Golikipa wa timu ya JKT Oljoro Damas Kugesha.

Wachezaji wa timu ya Prison pamoja na wachezaji wa timu ya JKT wakihaha katika lango la timu ya JKT baada ya kupigwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Mashambulizi yalielemea kila upande huku Prison ikionesha kuumiliki mnpira zaidi kuliko wageni lakini bahati haikuwa yao kwani kila wachezaji wa Prison walipokaribia goli la JKT aidha mpira ulikuwa unapigwa nje au golikipa wa JKT aliondosha hatari langoni.

Hadi timu zinatoka mapumziko JKT Oljoro ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0

Kipindi cha Pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo wenyeji Prison walimtoa Peter Michael na kumuingiza Ibrahimu Isaka na timu ya JKT iliwatoa wachezaji  Hamis Maulid na kumuingiza Sanu Mwasyeba na Beno Alfred aliingia badala ya Babu Ally.

 


Tofauti na ilivyozoeleka katika mechi nyingine mashabiki walikuwa wachache ambapo katika jukwaa ambalo wanapendelea kuketi mashabiki wa Mbeya City sehemu kubwa ilikuwa wazi na kuufanya mchezo huo kukosa hamasa kama ilivyozoeleka katika jiji la Mbeya.

Mashambulizi mengi yalioyofanywa langoni mwa timu ya JKT Oljoro hayakuweza kuzaa matunda na hivyo kuwapa wakati mgumu wachezaji wa Prison ambao walionekana kuhaha uwanja mzima kutafuta bao la kusawazisha.

Golikipa wa JKT Damas Kugesha alionekana kuwa na kazi nzito ya kuchomoa mikwaju ya wachezaji wa Prison.




Mara kadhaa mwamuzi Zakaria Jacob alionekana kuwa mkali kwa kuwazawadia kadi ya njano wachezaji ambao walionekana kucheza kabumbu isiyostahili

Hali haikuwa nzuri kwa timu ya Prison kutokana na wachezxaji wa JKT kuonekana kudhibiti kila eneo la uwanja kwani kKila alipokuwa mchezaji wa Prison walitokea wachezaji wawili wa JKT.

Wachezaji wa Prison mara nyingi walionekana kushindwa kulifikia goli la JKT kutokana na wachezaji hao kuwa wepesi kukimbia huku na kule na hivyo kuwapa kazi nzito maafende wa Prison.

Kila alipokuwepo mchezaji wa Prison walitokea wachezaji wawili au watatu wa JKT uchezaji huu wa timu ya JKT Oljoro uliwapa wakati mgumu wachezaji wa Prison na kujikuta wakishindwa kufurukuta hadi mwisho wa mchezo.




Mara nyingine wachezaji wa JKT walikuwa wakitumia mbinu za kimpira za kupumzika ama kupoteza muda kama inavyoonekana pichani golikipa wa timu ya JKT Damas Kugesha akigangwa na daktari wa timu yake huku mwamuzi wa mchezoZakaria Jacob akiangalia saa yake.


Mbali na maelekezo kutoka kwa mwalimu wao Alex Mwamgaya wachezaji wa JKT oljoro hawakuacha kupeana mikakati kila mpira uliposimama kwa muda



Ni kama bahati mbaya kwa mwalimu wa timu ya Prison David Mwamwaja ambaye amekabidhiwa kikosi hiki muda mfupi baada ya timu hiyo kuchabangwa mabao 2-0 na wadogo zao Mbeya City juma lililopita.



Kocha wa Prison Mwamwaja akitoa utetezi wake mbele ya waandishi wa habari sababu za kushindwa kwa mechi hiyo na kuahidi kujipanga katika mechi zijazo.

Kwa upande wake mwalimu wa timu ya JKT Oljoro Alex Mwamgaya kwake ilikuwa ni furaha kutokana na ushindi ulioipata timu yake.


Kama ilivyo desturi mashabiki wa timu ya Prison walijikuta wakikosa uvumilivu na kuingia uwanjani huku wakiimba nyimbo za kuutaka uongozi wa timu ya Prison uikabidhi timu hiyo kwa wananchi ikiwa inahitaji kufanya vizuri katika mechi zilizosalia.

Mashabiki hao walisikika wakisema kuwa, ''Mashabiki!!! tunaitaka!!! Timu Mashabiki tunaitaka Timu!!! ambapo mbali na kutaka wakabidhiwe timu walidai kuwa kuna mkono wa mtu katika uwanja huo kwani timu yao kila inapocheza na timu yoyote inashindwa kufanya vizuri katika uwanja huo, mshabiki mmoja alisikika akisema kuwa uwanja huo unatakiwa kufumuliwa kuondoa ndumba zilizozikwa ambazo anadai zinasababisha kushindwa kwa timu yao.



Kilio cha mashabiki wa timu ya Prison ni kuutaka uongozi ukabidhi timu kwa wananchi kama wanavyoonekana pichani.

Post a Comment

Post a Comment