Mwandishi wa habari Ezekiel Kamanga akiinua pikipiki baada ya kugongwa na gari ambayo ilikatisha ghafla kushoto katika eneo la Mabatini leo saa 5 asubuhi wakati tukifuatilia tukio moja huko Nzovwe. |
Msamaria mwema akisadia kuinua pikipiki baada ya mimi kuruka kutoka kwenye hiyo pikipiki na kuanza kupiga picha za ajali hiyo, tulikuwa tukifuatilia tukio moja eneo la Nzovwe. |
Gari hii ndiyo iliyotaka kubadilisha historia yetu leo hii asubuhi |
Dereva wa gari lililotaka kubadilisha historia ya maisha yetu leo hii mwenye tisheti ya Bluu bahari na jinzi akiomba msamaha kwa kosa alilolifanya kukatisha barabara ghafla na kutugonga. |
Wasamaria wema hawakuchelewa kuja kutoa msaada eneo la tukio kila mmoja akitupa pole kwa tukio lililotusibu |
Wasamaria wema wakiangalia ubovu wa pikipiki baada ya kugongwa na gari eneo la Mabatini leo asubuhi |
Jamaa wakicheki ubovu wa pikipiki |
Askari wa usalama barabarani naye hakuchelewa kufika eneo la tukio na kumuamuru dereva ageuze gari na kuliweka pembeni kwa maelezo zaidi. |
Hii ndiyo gari iliyotugonga leo hii wakati tukielekea eneo la Nzovwe kufuatilia kero za kijamii. |
Post a Comment
Post a Comment