NAWASHUKURU NDUGU ZANGU, NILIOWAKOSEA NAWAOMBA RADHI!!
KWA NIABA YANGU NA FAMILIA YANGU, NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU NA 
WAZAZI WANGU WALIONILETA DUNIANI NA KUNILEA AMBAO KWA SASA BAADHI YAO 
WAKO MBELE YA HAKI KWA KUNIJAALIA KUKARIBIA KUFIKISHA NUSU KARNE,NAAMINI
 WANGEKUWEPO WOTE LEO HII, NINGEJIFANYA MTOTO NA KUKETI KARIBU NAO, 
NINGEWAITA KWA MAJINA YAO ADHIIMU TULIYOZOEA KUWAITA, BABAA!!! MAMAAA!! 
NA WANANGU WANGEWAITA!! BABUUU!!! BIBII!!! LAKINI BAHATI MBAYA NIMEKOSA 
FURSA HIYO,NITAJITAHIDI KUWAENZI JAMAA NA MARAFIKI WA WAZAZI WANGU 
NAAMINI KWA KUFANYA HIVYO THAWABU ITAWAFIKIA WALIKO MBELE YA HAKI,HATA 
HIVYO BADO NAMTHAMINI MAMA YANGU ALIYOKO SASA NAMPENDA NA KUMJALI KWA 
KUWA ANANIPENDA NA KUNIJALI, AMENILEA NA KUNIKUZA HADI NIMEFIKIA UMRI 
HUU, SINA LA KUMLIPA, BADO NAKUTHAMINI MAMA YANGU, MUNGU ATAKUPUNGUZIA 
MARADHI YA UTU UZIMA, NAAMINI ANGEKUWEPO BABA YANGU LEO HII UNGEKUWA 
KAMA BADO NI KIJANA, NAWASHUKURU NDUGU NA JAMAA ZANGU NINAOISHI NAO KWA 
SASA HUKU UGHAIBUNI, MBALI NA NILIKOZALIWA,MBALI NA CHANGAMOTO LUKUKI 
NINAZOKUTANA NAZO KATIKA JAMII NIISHIYO, BADO TUNASAMEHEANA NA MAISHA 
YANASONGA MBELE, NAWAOMBA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ZANGU MUENDELEE 
KUNISAMEHE KW AMAKOSA NIYAFANYAYO AMBAYO NI YA KIBINADAMU, MAANA HAKUNA 
BINADAMU MKAMILIFU, NAMI NACHUKUA FURSA HII KUWASAMEHE WALIONIFANYIA 
INDA, KWANI NAAMINI ALIYEKAMILIKA NI MWENYEZI MUNGU PEKEE, NI VIGUMU 
KUWATAJA MMOJA MMOJA KATIKA ORODHA NDEEFU YA MARAFIKI ZANGU, BALI KWA 
UMUHIMU WA KIPEKEE,NAWASHUKURU BLOGERS WOTE WA NDANI NA NJE YA 
NCHI,WANAHABARI WOTE WA NDANI NA NJE YA NCHI AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA 
NYINGINE TUMEKUWA TUKIBADILISHANA MAWAZO KUPITIA KALAMU ZETU, AIDHA 
NAISHUKURU KAMPUNI YA UCHAPISHAJI MAGAZETI YA BUSINESS TIMES, INAYOTOA 
MAGAZETI YA MAJIRA,BUSINESS TIMES,SPOTI STAREHE NA MAISHA, PIA REDIO 
TIMES FM YA JIJINI DAR AMBAO WOTE KWA PAMOJA WAMENIPA NGUVU YA KUKUTANA 
NA JAMII ILIYOMBALI AMBAO WAMEKUWA WAKIZISOMA NA KUZISIKIA KAZI ZANGU 
KUPITIA VYOMBO HIVYO, NAWASHUKURU PIA WASOMAJI WA MAKALA NA KAZI ZANGU 
AMBAO WAMEKUWA WAKINISAPOTI KWA KUNIPIGIA SIMU BAADA YA KUZISOMA KAZI 
ZANGU, PIA NAWASHUKURU WADAU WENGINE KAMA VILE TAMWA,TMF,HAKI 
ELIMU,TGNP,MISA-TAN,GEMSA,MCT,UTPC NAWENGINE AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA 
NYINGINE WAMEKUWA WAKIZIJALI KAZI ZANGU NA KUZIFANYIA KAZI, PIA KWA 
UPEKEE NAWASHUKURU WAHARIRI MBALIMBALI NILIOWAHI KUFANYA NAO KAZI, 
MAGAZETINI, WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI 
MKOA WA MBEYA, AMBAO KUTOKANA NA MSUKUMO HUO NIMEFANIKIWA KUWA MIONGONI 
MWA WANAHABARI 76 WENYE KAZI 101 AMBAZO ZINAWANIA TUZO YA EJAT, 
ITAKAYOFANYIKA KESHOKUTWA JIJINI DAR, NAAMINI HII NI FURSA PEKEE YA 
KUADHIMISHA UMRI NILIOUFIKIA KWA FURAHA, RAHA NA FARAJA, KWANI MIE SINA 
UJANJA WA KUNIWEZESHA KUFIKISHA UMRI HUO, NI MUNGU PEKEE, KANICHANGUA 
MIONGONI MWA WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI ILI NIBAKI NISHUHUDIE 
MALIMWENGU YANAYOTOKEA, SINA LA KUSEMA ZAIDI YA KUMSHUKURU KWA KUSEMA 
ALHAMDULILLAHI!!!
Post a Comment