|  | 
| Baadhi yao walishindwa kuhimili joto hilo lililoambatana na njaa na hivyo kulazimika kukaa chini ya mvungu wa gari ili kujisitiri na jua. | 
|  | 
| Hali ilipokuwa mbaya baadhi yao walilazimika kuhemea vyakula katika vijiji vya jirani na kuamua kuchukua majiko yao ya mkaa kwa ajili ya kuandaa msosi kama picha zinavyojidhihirisha. | 
|  | 
| Umati wa abiri walioshuka kwenye magari yanayokadiriwa kufika 1000 waendao na wale watokao Dar walishuka na kuhaha huku na kule bila kupata ufumbuzi wa safari yao. | 
|  | 
| Baada ya kugongana gari hilo lilikatisha njia na kuzuia magari yote yaliyokuwa yakielekea na kutoka Dar es salaam. | 
|  | 
| Baadhi ya wananchi walijityokeza kutoa msaada wa kulisukuma gari lililozuia barabara na kusababisha msongamano | 
|  | 
| Baadhi ya abiria walishindwa kuhimili joto kutokana na jua kali na kukata kiu kwa kunywa maji na juise kama anavyoonekana abiria huyu pichani | 
|  | 
| Msururu wa magari yalishindwa kuendelea na safari na hivyo kila gari lililofika eneo hilo lilijikuta likisimama kusubiri utaratibu wa kuondoka eneo hilo | 











Post a Comment