Mkurugenzi wa Binslum Company Mohamed Binslum akiangalia jezi zenye mwonekano mpya za timu ya Mbeya City huku Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya akiangalia |
Mkurugenzi wa Binslum Mohamed Binslum akisoma taarifa za mkataba wa udhamini baina ya kampuni yake na timu ya Mbeya City |
Meneja wa Timu ya Mbeya City Emmanuel Kimbe akishikana mkono wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Binslum ya Jijini Dar es salaam ambao wameidhamini timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili wa sh. milioni 360 |
Baadhi ya wanahabari wakijadiliana wakati wa halfa fupi ya utiaji saini ya udhamini wa klabu ya Mbeya City leo asubuhi |
Timu Meneja wa Mbeya City Emmanuel Kimbe |
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro |
Mkurugenzi wa kampuni ya Binslum, Mohamed Binslum |
Add caption |
TIMU ya
Mbeya City ambayo ilicheza Ligi Kuu msimu kwa mafanikio makubwa jana imepata
udhamini mnono wa sh.milioni 360 kwa miaka miwili kutoka kampuni ya Binslum ya Jijini Dar es salaam.
Mbeya City
iliyojizolea sifa lukuki kwa mtindo wake wa kuzidindia timu zote zilizocheza
ligi Kuu msimu uliopita imewashawishi wadhamini hao kuwekeza kwa timu hiyo kwa
nia ya kuongeza chachu kwa timu za mikoani zinazocheza Ligi Kuu.
Akizungumza wakati
wa utiani saini wa mkataba huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji leo asubuhi, Mkurugenzi
wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum alisema udhamini wao umelenga kuleta
changamoto na hamasa kwa timu za mikoani.
Binslum
alisema kuwa wameamua kuwekeza kwa Timu ya Mbeya City kutokana na namna ambavyo
timu hiyo imeonesha mtindo wa kipekee wa ushawishi kwa soka hapa nchini kinyume
na ilivyozoeleka kwa timu kubwa za Yanga na Simba.
Alisema kuwa
kampuni ya Binslum inaamini itanufaika kwa kutangaza bidhaa zake kupitia jezi
za timu hiyo katika michezo yake kwa msimu wa mwaka 2015-16 na kuwa wamefikia
makubaliano hayo na uongozi wa Mbeya City kutokana na mwitikio mkubwa wa
wapenzi wa soka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo fupi ya utiaji saini mkataba na kampuni hiyo
Meneja Mbeya City Emmanuel Kimbe alisema kuwa anaamini ufadhili huo utachangia
kuiongezea uwezo timu hiyo katika ligi Kuu msimu ujao wa 2015 na 2016.
Alisema kuwa
mkataba huo utachangia kuongeza kipato cha timu hiyo na kuiwezesha kujikimu kwa
matatizo madogo madogo ambayo anaamini yatatatuliwa kwa ufadhili huo wa miaka
miwili.
Naye Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambaye ndiye mmiliki wa timu hiyo Dkt. Samwel
Lazaro alisema kuwa ufadhili kwa timu za mikoani utachangia klabu nyingi zisizo
na uwezo wa kifedha kushiriki ligi kwa ushindani katika ligi na kukua kwa soka
la Tanzania.
Post a Comment
Post a Comment