|  | 
| Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid | 
Na Kibada Kibada, Katavi 
Mkoa wa
Katavi  kupitia sekta ya Afya  umewapatia watumishi   wa sekta hiyo wapatao 240  mafunzo  ya namna ya kutoa huduma ya Tiba  ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Mganga Mkuu
wa  Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Husein  ameeleza kuwa watumishi hao 240 waliopatiwa
mafunzo ni sawa na asilimia 100 ya lengo lililowekwa  kuwapatia mafunzo ya huduma hiyo mkoani.
Akifafanua
zaidi  Dkt. Husein amesema kuwa  hadi kufikia mwezi juni mwaka 2014 jumla ya
vituo 61 sawa na asilimia miamoja na ishirini ya lengo  la vituo 51 vinatoa huduma hii katika Mkoa wa
Katavi.
Amesema kuwa
 ili kufanikisha adhima ya shirika la
Afya Duniani la kuthibiti maambukizi toka kwa mama mwenye  VVU kwenda kwa Mtoto,Wizara ya Afya
ikishirikiana na wadau wa Maendeleo imeanzisha huduma ya Tiba ya kuzuia  maambukizi toka kwa Mama mwenye VVU kwenda
kwa Mtoto.
‘’Akina mama
wajawazito wanaonyonyesha wakigundulika kuwa wana maabukizi ya UKIMWI
wataanzishiwa tiba ya kudumu’’alisema.
Aidha kama
Mkoa utahakikisha huduma hii inatolewa katika vituo vyote vinavyotoa huduma ya
Afya ya Uzazi.
Kuhusu
huduma   inayotolewa 
amesema ni bora ,timu ya Afya Mkoa 
na Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo katika sekta ya
Afya Walter Reed zitaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi elekezi kila
mwezi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Programu ya Shirika la  Walter Reed Dkt Joseph Chintowa ameeleza kuwa
Shirika lake kwa kushirikiana na  wadau
wa wote wa Mkoa,Wilaya,Halmashauri na Mji wa Mpanda wanasaidia juhudi za
Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Dkt Chintowa
ametoa wito kwa akina Baba kupima afya  pamoja na wake zao ili kujenga  familia zenye afya bora na ya uhakika,ambapo
pia amewaasa wazazi kukumbuka dhamana waliyonayo juu ya kuwakinga watoto wao na
maambukizi ya UKIMWI.


Post a Comment