Ads (728x90)

Tulipata fursa ya kukutana na marafiki wapya walitufurahia ujio wetu nchini mwao, tulikuwa kama watalii wa kutokea nchini Tanzania waliokwenda kujifunza mambo ya nchi za wenzetu, tulikutana na watalii wenzetu kutoka nchi mbalimbali, za Ulaya tukaunda urafiki tukabadilishana mawasiliano na kukubaliana baadhi ya mambo ikiwemo kutembelea nchini kwao na wao kutembelea nchini mwetu.
Tulikutana Watalii kutoka Tanzania na Watalii kutoka nchi za Ulaya tukawa kitu kimoja kwa malengo yanayofanana kwa ziara tofauti.
Pia tulikutana na Watanzania na marafiki zetu waishio nchini Malawi wakatuelekeza nam,na ambavyo wanaishi vyema na wenyeji wao na namna ambavyo wamefanikiwa kimaisha. hapa mdau mkubwa wa habari Mohammed Hassan akiwa na Classmate wake waliyesoma naye katika shule ya Sekondari Sangu nchini Tanzania Brandy Nelson.

Ndugu zetu na wanahabari wenzetu wa Mzuzu nchini Malawi walituunga mkono kwa asilimia zote hapa Kiongozi wa Msafara Ulimboka Mwakilili akiteta jambo na Mweka hazina wa Nyika Media Club ya Jijini Mzuzu  Sarah Munthali

Tulipata marafiki ambao ni watalii kutoka nchi za Ulaya ambao tulibadilishana mawazo na kukubaliana baadhi ya mambo kwa mustakabali ya baadaye




Rais wa Chama Cha Waandishi wa habari wa Mzuzu Nyika Media Club Chimbizga Msimuko alikuwa mstari wa mbele kutupokea na kutupa ushirikiano wa kila hali

 

Post a Comment

Post a Comment