| Mmoja wa moderator wa Mbeya Yetu wamiliki wa Blog za Mikoa Fred Njeje akiwa katika pozi kwenye moja ya baiskeli ambazo hutumika kusafirisha abiria nchini Malawi. | 
| Jiji la Lilongwe lilianza kuonekana baadhi ya mitaa yake tunapoingia mjini. | 
| Tulikutana na mwenyeji wetu mwandishi wa habari wa Malawi Francis Tayanja Phiri akatulaki kwa furaha na kutukaribisha yeye alisafiri kutokea Blantyre na kuingia Lilongwe dakika 20 zilizopita. | 
| Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Raia Mwema Felix Mwakyembe akisalimiana na nguli wa habari nchini Malawi Francis Tayanja Phiri Jijini Lilongwe nchini Malawi. | 
| Ilikuwa ni furaha kubwa kukutana na mwenyeji wetu mara tukaanza kubadilishana mawazo na kupeana taarifa za safari yetu ndefu kutokea nchini Tanzania, kupitia Karonga, Mzuzu hadi Lilongwe. | 
| Mwandishi wa habari Francis Tayanja Phiri akitoa taarifa fupi ya ratiba ya siku inayofuata kwa waandishi wa habari kutokea nchini Tanzania. | 
| Baada ya kikao cha muda mfupi tulikutana kwa ajili ya chakula cha jioni katika Hoteli moja iliyopo jirani na mahala tulipofikia. | 
| Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Brandy Nelson akitahayari na kutafakari juu ya aina ya maisha waishio majirani zetu wa nchini Malawi, hapa ilikuwa ni katika Klabu ya Usiku. | 
| Brandy Nelson mwandishi wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania | 
| Fred Njeje Moderator wa Mbeya Yetu Blog na Blog za Mikoa akijivinjari katika Klabu ya usiku Jijini Lilongwe nchini Malawi. | 
Post a Comment