| Njiani tulishuhudia namna ambavyo Mwenyezi Mungu alivyoumba dunia kwa kuweka milima iliyofanana na vigingi vilivyosimikwa ardhini kuisimamisha dunia. | 
| Tulisafiri kwa mwenda mrefu tukasimama kuchimba dawa katika baadhi ya nyumba katika kijiji kimoja cha Luwawa wilayani Mzimba mkoa wa Kaskazini. | 
| Baadhi ya nyumba za maeneo haya kijiji cha Luwawa WILAYA ya Mzimba nchini Malawi ni sawa na baadhi ya nyumba za vijiji vya TANZANIA | 
| Tulivutiwa na uchomaaji wa mbuzi kwa njia ya kukaanga kwenye karai tulitafuna nyama ya mbuzi kutuliza njaa | 
| Tulifika katika mji maarufu wa Jenda hapo tulipata fursa ya kupumzika kidogo, ni safari ya kuelekea Jijini Lilongwe, ilikuwa ni safari nzuri ya kuvutia. | 
Post a Comment