|
Mabaki ya gari aina ya Land Cruiser mali ya Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF baada ya kutokea ajali eneo la Old Vwawa wilayani Mbozi jana asubuhi |
|
Mke wa marehemu Said Mkumba akisaidiwa baada ya kushuhudia ajali iliyosababisha kifo cha mumewe |
|
Gari la NSSF lililowabeba Kaimu Meneja na dereva wake baada ya kugongana uso kwa uso la Lori |
|
Hivi ndivyo ilivyokuwa jana katika eneo la ajali baada ya dereva wa Lori kunasuliwa kwenye Chases alikobanwa |
|
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu mjini Vwawa wilayani Mbozi wakiomba dua kabla ya kuanza kwa safari ya kuwasindikiza marehemu waliofariki katika ajali |
|
Magari yaliyobeba miili ya marehemu yakijiandaa kwa safari ya kuelekea Chalinze na Dar es salaam kwa ajili ya mazishi |
|
Buriani!! Kwa heri ya kuonana |
|
Gari lililobeba mwili wa Kaimu Meneja wa NSSF Said Mkumba likianza safari |
|
Baadhi ya wakazi wa mjini Vwawa wakitawanyika baada ya kuaga miili ya waliokufa kwa ajali |
Miili ya wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF) Wilayani Mbozi mkoani Mbeya imeagwa na kusafirishwa leo kuelekea mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu hao ni kwamba mwili wa Said Mkumba ambaye alikuwa Kaimu Meneja wa NSSF wilayani Mbozi unasafirishwa kuelekea Mbagala Jijini Dar es salaam huku mwili wa aliyekuwa dereva wa gari hilo Mbaraka Kiwamba unasafirishwa kuelekea Chalinze mkoani Pwani.
Baadhi ya wakai wa mjini Vwawa, walishiriki kuaga miili ya marehemu hao katika mtaa wa Ilolo na Ichenjezya majira ya saa sita mchana.
Ajali hiyo ilitokea jana mnamo majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Old Vwawa kwenye mteremko wa barabara ya Mbeya Tunduma.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba chanzo cha ajali hiyo kilitokana na Lori la Mafuta ambalo lilikuwa linaelekea mjini Tunduma kugongana uso kwa uso la Landcruiser ya NSSF ambapo mbele yake kulikuwa na magari yaliyokuwa yakisindikiza harusi.
Taarifa zinaeleza kuwa Land Cruiser ilikuwa inatokea Tunduma kuelekea Vwawa ilhali Lori lilikuwa linaelekea Tunduma nyuma ya magari yaliyokuwa kwenye msafara wa harusi ambao ulikuwa unaelekea njia ya Tunduma.
Inaelezwa kuwa Dereva wa Lori aliyefahamika kwa jina la Maduhu aliamua kuovateki msafara wa magari ya harusi ndipo alipokutana uso kwa uso na Landcruiser ambayo ilikuwa katika upande wake ikielekea mjini Vwawa na kusababisha vifo vya Mkumba na Kiwamba ambao wapoteza maisha papo hapo.
Mara baada ya kugongana uso kwa uso na LandCruiser Lori hilo lililobeba mafuta aina ya Petrol lilipinduka bondeni upande wa kulia ambapo dereva wake alibanwa kwenye Chesesi ya gari hilo na kuchomolewa baada ya masaa matano tangu kutokea kwa ajali hiyo.
Post a Comment
Post a Comment