MSHITAKIWA wa usafirishaji wa Mirungi(wa pili kutoka kulia) akiwa katika gari la Polisi akipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana |
Washitakiwa wa makosa mbalimbali wakipelekwa mahabusu jana wakitokea kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbozi |
Mshtakiwa wa makosa ya usafirishaji wa Mirungi Joram Mwakalebela akielekezwa na askari kanzu kukaa chini baada ya kuahirishwa kwa kesi inayomkabili ya kukutwa na Mirungi kilo 80. |
MSAFIRISHAJI
maarufu wa mirungi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati Joram Mwakalalebela(48)(Sabas)
ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya baadaye kufikishwa katika
mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Mbozi kwa tuhuma za kukutwa na mirungi kilo
80.
Inadaiwa
kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa njiani kuelekea nchi za Zambia hadi nchini DRC
ambako amekuwa akifanya biashara ya usafirishaji mirungi kwa zaidi ya miaka 10.
Mwakalebela(48)
ambaye ni mkazi wa Forest Jijini Mbeya amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilayani Mbozi mkoani Mbeya kwa kosa la kukutwa na
dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 80.
Akisoma
mashtaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbozi Rahimu
Mushi, mwendesha Mashtaka wa Polisi Inspekta Samweli Sarro alisema kuwa
mshtakiwa alifanya kosa hilo Januari 24 mwaka huu.
Alisema
mshtakiwa alikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Jabari iliyopo Sogea mjini
Tunduma majira ya saa 3:30 asubuhi akiwa na dawa za kulevya aina mirungi ikiwa
katika mafungu 250 sawa na kgm 80.
Hata hivyo
mshtakiwa alikana kosa hilo na kurejeshwa rumande hadi Februari 10 ambapo
alipewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye nyumba zisizohamishika na
fedha taslimu kiasi cha sh. milioni 5.
‘’Alikutwa
katika nyumba ya kulala wageni ya Jabari ipo kitongoji cha Sogea mjini Tunduma,
mirungi ilikua katika vifurushi vya mafungu 250 ni sawa na kilo 80,’’alisema
Inspekta Sarro.
Kwa mujibu
wa baadhi ya wakazi wa mjini Tunduma wanadai kuwa kilo moja ya Mirungi ni sawa n
ash.40,000 hivyo kiasi hicho cha mirungi kilichokamatwa ni zaidi y ash. Milioni
3.
Post a Comment