Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadharani mjini Tukuyu wilayani Rungwe jana. |
Mamia ya wakazi wa mjini Tukuyu wakimuunga mkono Mwenyekiti wa CHADEMA kutosogeza mbele uandikishwaji wa wapiga kura ulianza kuendeshwa kwenye baadhi ya mikoa nchini |
Baadhi ya wakazi wa Ushirika Kata ya Mpuguso wilayani Rungwe wakiwa wamelala barabarani kumsubiri Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. |
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu akihutubia mkutano kabla ya kumkaribisha Mbowe katika viwanja wa Tukuyu wilayani Rungwe jana. |
Mbowe akishuhudia uandikishwaji wa wapiga kura katika kituo cha Mpuguso wilayani Rungwe. |
Mmoja wa wazee wa kijiji cha Mpuguso akiwa amelala chini kuonesha ishara ya upendo na utiifu mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. |
Hii ni kauli
ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo “CHADEMA”Freeman Mbowe
aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji wa
Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya, juzi jioni.
Mbowe ambaye
pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro
aliyasema hayo kwa niaba ya viongozi wa Muungano wa UKAWA akiwataka wananchi wa
wilayani Rungwe kujitokeza kujiandikisha katika daftari la Wapiga kura ambalo
pia alisema limegubikwa na dosari nyingi.
Alisema kuwa
ana uhakika mkubwa wa UKAWA kuiong’oa CCM madarakani Oktoba mwaka huu na
kuwataka viongozi waliopo madarakani kutubu kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwadhulumu
Watanzania na kuwa katu wao hawatalipiza kisasi kwa matendo yao kwa Watanzania.
‘’Hii si
nchi ya kulipizana kisasi bali tunapaswa kuangalia mambo ya msingi ya kutujenga
sote badala ya kupoteza muda wa kulipiza kisasi kwa makosa ya wachache,’’alisisitiza
Mbowe.
Alidai kuwa
kuna kila dalili za hujuma dhidi ya uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari
la kudumu kwa kuwa zoezi limefanywa kwa kupoteza muda bila sababu za msingi
jambo ambalo lilipaswa kufanywa kila baada ya miaka mine.
Alisema kwa
kipindi cha zaidi ya miaka saba hakukuwa na mchakato wowote wa uboreshaji wa
daftari hilo na kutegea zikiwa zimebaki siku chache ili kuwe na sababu za
kusogeza mbele uchaguzi mkuu jambo ambalo UKAWA hawako tayari kukubali.
‘’Hatutokubali
kusogezwa mbele uchaguzi mkuu hata kwa siku moja, tunaomba Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ifanye iwezavyo ili asiwepo mwananchi mwenye haki ya kujiandikisha
akakosa fursa hiyo’’alisema.
Aidha Mbowe
aliwaasa watia nia wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho
kugombea nafasi zao kwa nia ya kweli badala ya kutanguliza ubinafsi na kuwa
chama hicho hakitawapokea wagombea wanaotanguliza maslahi binafsi.
Alisema
viongozi waliotia nia wanapaswa kufuata Katiba ya chama hicho na kwamba yeyote
atakayekiuka katiba hatovumiliwa na chama hicho kwa kuwa kinajengwa wenye nia
thabiti ya kuwatumikia Watanzania.
Alibainisha
kuwa chama hicho hakina ubinafsi kama ilivyoenezwa propaganda dhidi yake na
kuwa kama kungekuwa na ubinafsi yeye Mbowe angekuwa mtu wa kwanza kukihodhi
chama hicho kwa kuwa ametumia fedha zake za mfukoni kukifikisha hapo kwa zaidi
ya miaka 20.
‘’Kama
kungekuwa na ubinafsi mimi Mbowe ningesema chama hiki ni mali yangu, nimetumia
rasilimali fedha zangu kutoka mfukoni mwangu na kukifikisha hapa kilipo,’’alisema
na kuongeza.
‘’CHADEMA ni
sawa na treni ambayo abiria wake ni wavumilivu,wako wanaokosa uvumilivu ambao
hushukia njiani hawa ni wale wanaokiuka Katiba ya chama chetu,’’alisema.
Mbowe ambaye
aliambatana na wabunge wanne wa chama hicho Joseph Mbilinyi(Mbeya mjini) Rebeka
Mngondo (Viti maalumu Arusha)Cesilia Pareso(Arumeru) na Naomi Kaihula (Viti
maalum Mbeya) wamefanya ziara mkoani Mbeya na kutembelea wilaya za Rungwe na
Kyela ambako zoezi la uandikishaji wapiga kura linaendelea.
Post a Comment