Ads (728x90)

Huduma duni za kijamii kwa wananchi waishio vijijini hushabihi mazzingira halisi waishiyo na kuathiri maisha halisi ya wakazi wa maeneo mengi ya vijijini, Pichani mwanamke Mkazi wa kijiji cha Chimbuya wilayani Mbozi mkoani Mbeya akiwa ameambatana na wanayewakipita huku na huko  kusaka maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama alivyonaswa na kamera yetu juzi.
Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Marcus Mwoga(12) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Chimbuya akiwa amebeba kifurushi cha mahindi wakati wa masomo  kuelekea mashine ili asage unga wa kula nyumbani, mashine hiyo ya kusaga ipo umbali wa kilomita tatu.

Baadhi ya maeneo ya wakazi waishi pembezoni mwa barabara kuu wamekuwa wakinufaika kwa usafirishaji rahisi wa mazao yao kutokea vijijini kama inavyoonekana pichani gari aina ya Pick Up ikiwa imesheheni mizigo ya mazao kutokea vijijini ikipita katika barabara kuu ya Tanzania Zambia maeneo ya Hanseketwa wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Watoto wengi waishio vijijini wamekuwa wakikosa hamasa ya masomo kutokana na ukata wa maisha ya walezi wao kama inavyoonekana pichani, watoto hawa wa familia moja Damian Kibona na Richard Kibona wanafunzi wa darasa la Nne na la pili katika shule ya Msingi Mwenge iliyop[o Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya wakichuma malimao kwa ajili ya kuuza ili kujipatia fedha za kujikimu.





Post a Comment