Mkurugenzi
wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza
kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo
Supaset 42.5”leo Oktoba 12, 2015 katika ofisi zao jijini Dar es Salaam.
Anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine
Langreney pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga. Picha zote
na Cathbert Kajuna.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati)
akishangilia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge
Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) pamoja na akiwa na Mkurugenzi
wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga mara baada ya uzinduzi wa chapa mpya ya
saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza
kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo
Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na
Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao
jijini Dar es Salaam. ambapo alisema Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti
makini uliofanywa na wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi
mahitaji ya soko.
Waandishi wa habari pamoja na wageni walioungana katika uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5”
---
Ikiwa
ni jitihada mahususi kuwapa saruji imara zaidi wakandarasi na
wafyatuaji matofali Lafarge Tanzania imezindua chapa mpya ya saruji
iitwayo “Tembo Supaset 42.5” ambayo ni imara na mahususi kwa ufyatuaji
matofali, zege, majengo makubwa pamoja na miradi mikubwa ya miundombinu
kama madaraja, barabara na majukwaa ya michezo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania,
Catherine Langreney alisema kwamba Tembo Supaset 42.5 ni saruji maalum
iliyobuniwa ili kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya saruji imara na
inayokauka haraka katika soko la ufyatuaji matofali na zege na ujenzi
mkubwa “Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na
wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya
soko.”alisema.
Akizungumzia
kuhusu maendeleo katika sekta ya ujenzi Langreney alisema kwamba kwa
ujumla thamani ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania inakadiriwa kuwa dola
bilioni. Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 7.8 mwaka 2014 na ni sawa na
asilimia 8.6 ya pato la taifa ikiwa ni kutokana na ujenzi binafsi,
usafirishaji na miradi mikubwa ya ujenzi. Tanzania ina idadi ya zaidi ya
milioni 44 kufikia mwaka 2014 na inatarajiwa kuongezeka sambamba na
ongezeko la mahitaji ya nyumba na miundombinu.”
Mkurugenzi
wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo alisema kuwa
Tembo Supaset ambayo itauzwa kwenye soko la jumla na rejareja ikiwa
katika ujazo wa kilo 50 ni saruji imara zaidi ikiwa na ubora kuliko
saruji nyingine zilizopo kwenye soko kutokana na uimara pamoja na bei
shindani ambazo zimepangwa na itakidhi mahitaji ya watumiaji kama vile:
• Kuimarika mapema jambo ambalo litawaongezea tija wazalishaji bidhaa zinazotokana na zege
• Ukaukaji wa haraka jambo litakaloyafanya matofali yaweze kuhamishika haraka na kuongeza tija wazalishaji
• Mchanganyiko mzuri wa zege na matumizi kidogo ya maji kuimarisha.
Chonjo
alisema kwamba Tembo Supaset imezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko
kuwa na saruji imara zaidi huku akitarajia saruji hyo kupanua soko la
Lafarge Tanzania hususani kwa wafyatuaji ambao hutegemea saruji
inayoimarika haraka katika kazi yao. “Mbali na uimara, faida nyingine ya
Supaset ni kuweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa na maana kwamba majengo
yatakayojengwa kwa saruji hiyo yatadumu zaidi”
Alisema
neno Supaset linamaanisha uimara kutokana na kukauka mapema na kukaa
muda mrefu zaidi katika uimara na saruji hiyo ni sehemu ya saruji za
chapa ya Tembo.
Post a Comment
Post a Comment