Kikosi cha Timu ya Prison ambacho narehemu Hassan Mlwilo aliwahi kukifundisha enzi za uhai wake.
ALIYEWAHI
kuwa kocha wa timu ya Prison na Mwalimu wa michezo wa Jeshi la Magereza nchini
Hassan Yassin Mlwilo(58) amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili
alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo aliyokuwa akisumbuliwa kwa takribani miezi
miwili iliyopita.
Kwa mujibu
wa Meneja wa timu ya Prison Athanas Kilindo aliyezungumza kwa njia ya simu na
mtandao huu alisema kuwa juma lililopita Mlwilo alifika jijini Mbeya na kulazwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na baadaye kuhamishiwa katika hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kilindo
alisema kuwa Mlwilo aliondoka Mbeya Januari 16 na kufariki Januari 21 majira ya
saa 5:30 mchana ikiwa ni siku tatu baada
ya kufika katika hospitali hiyo ya Muhimbili na kuwa mazishi yake yatafanyika
Ubaruku Rujewa wilayani Mbarali kesho majira ya saa 7:00 adhuhuri.
Alisema kuwa
Mlwilo alipata kufundisha timu mbalimbali za mkoa wa Mbeya ikiwa ni pamoja na
timu ya Tiger ya Tunduma na baadaye kuifundisha timu ya Prison kabla ya kuwa mwalimu
wa michezo wa Jeshi la Magereza.
‘’Tumempoteza
mdau muhimu wa michezo ndani ya Jeshi la Magereza alikuwa na uwezo mkubwa na
alijitikiza katika michezo yote, hadi anafariki alikuwa ni Ofisa michezo wa
Jeshi la Magereza,’’alisema Kilindo.
Mlwilo
ameacha mjane na watoto, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema,
Amiin!!!
Post a Comment