Ads (728x90)

Kikosi cha Timu ya Prison ambacho narehemu Hassan Mlwilo aliwahi kukifundisha enzi za uhai wake.

ALIYEWAHI kuwa kocha wa timu ya Prison na Mwalimu wa michezo wa Jeshi la Magereza nchini Hassan Yassin Mlwilo(58) amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa maradhi ya tumbo aliyokuwa akisumbuliwa kwa takribani miezi miwili iliyopita.
Kwa mujibu wa Meneja wa timu ya Prison Athanas Kilindo aliyezungumza kwa njia ya simu na mtandao huu alisema kuwa juma lililopita Mlwilo alifika jijini Mbeya na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na baadaye kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kilindo alisema kuwa Mlwilo aliondoka Mbeya Januari 16 na kufariki Januari 21 majira ya saa 5:30 mchana  ikiwa ni siku tatu baada ya kufika katika hospitali hiyo ya Muhimbili na kuwa mazishi yake yatafanyika Ubaruku Rujewa wilayani Mbarali kesho majira ya saa 7:00 adhuhuri.
Alisema kuwa Mlwilo alipata kufundisha timu mbalimbali za mkoa wa Mbeya ikiwa ni pamoja na timu ya Tiger ya Tunduma na baadaye kuifundisha timu ya Prison kabla ya kuwa mwalimu wa michezo wa Jeshi la Magereza.
‘’Tumempoteza mdau muhimu wa michezo ndani ya Jeshi la Magereza alikuwa na uwezo mkubwa na alijitikiza katika michezo yote, hadi anafariki alikuwa ni Ofisa michezo wa Jeshi la Magereza,’’alisema Kilindo.

Mlwilo ameacha mjane na watoto, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema, Amiin!!!

Post a Comment

Post a Comment