MKUU wa mkoa wa Mbeya
Amos Makalla amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi mkoani Mbeya kutenga
siku moja ya Alhamisi kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Makalla alitoa agizo
hilo wakati akizungumza kwenye mkutano uliowahusisha wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalama, madiwani,maofisa watendaji wa kata ,viongozi wa vyama vya
kisiasa, viongozi wa dini, machifu, wazee maarufu na watumishi wa halmashauri
ya wilaya ya Kyela.
Aidha Makalla amewapongeza wakuu wa
wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Mbeya kwa jitihada za kutokomeza
ugonjwa wa Kipindupindu na kuwa tangu Machi 27 mkoa wa Mbeya hauna mgonjwa hata
mmoja wa kipindupindu.
‘’Niliporipoti mkoani Mbeya Machi 17 niliwaagiza
MADC na wakurugenzi kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, tangu Machi 27 hadi
sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Kipindupindu,’’alisema Makalla.
Katika kuzingatia hali ya usafi Mkuu
huyo wa Mkoa wa Mbeya Makalla aliwataka wananchi kuzingatia kanuni za Afya
kuanzia ngazi ya kaya na kuhimiza kila kaya iwe na choo kizuri.
Pia katika kuhakikisha tatizo la
madawati linakoma mkoani Mbeya amewaomba Wabunge, madiwani na wananchi kwa kushirikiana
na wadau kuhakikisha tatizo la madawati linaisha ifikapo Mei 31 mwaka huu.
|
Post a Comment
Post a Comment