Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa kwenye kituo cha kupokea umeme |
Baadhi ya Wafanyakazi wa TANESCO wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza baadhi ya wateja wa Shirika la Umeme TANESCO jijini Mbeya |
ZIARA ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo imemfikisha Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na kuwataka watumishi wa shirika hilo kuacha kushirikiana na wezi maarufu wa umeme almaarufu Vishoka ambao wamekuwa wakiharibu sifa nzuri ya utendaji wa Shirika hilo nchini.
Makalla aliwataka watumishi hao kuboresha utendaji wao ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wateja ambapo aliuagiza uongozi wa shirika hilo kutoa huduma nzuri kwa kiwango cha kuridhisha.
Katika ziara hiyo pia alipata fursa ya kukagua kituo cha kupokelea umeme na kuzitaka taasisi zote za serikali zinazodaiwa na TANESCO kulipa madeni yao mara moja ili kuliongezea ufanisi wa utendaji Shirika hilo.
Kadhalika Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ambaye kwa muda mrefu amekuwa katika ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii amewataka wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini (REA) waongeze kasi na kumaliza kazi hiyo ifikapo Juni 15 mwaka huu kama walivyoelekezwa na Wizara.
Post a Comment
Post a Comment