Tamu ishindayo hamu, si tamu yenye ugumu,
Ni tamu yenye nidhamu, iletayo balaghamu,
Tamu ni tunu adhimu, na ladhaye ni adimu,
Hizi ndo tungo tamu, ziburudivyo uoni.
Zenye utungu si tamu, 'kukari' zaisha hamu,
Tungo zilizo hitimu, ztukuzwa na walimu,
Hutokwa umaamumu,na kutambia kaumu,
Hizi ndo tungo tamu ziburudivyo uoni.
Zilo murua nudhumu,hutakasisha kalamu,
Hu'kari' wenye ilimu, kwa kuchambua muhimu,
Tungo walotaqadamu, fani waliiheshimu,
Hizi ndo tungo tamu,ziburudivyo uoni.
Tungo ziso na nidhamu, fatahize si timamu,
Ni mithali ya sanamu, urari wake hanamu,
wengi wanotunga humu, huteza yalo lazimu,
Hizi ndo tungo tamu. ziburudivyo uoni.
Tungo zenye idghamu, 'amba' zina irhamu,
Hujiweka maalumu,hubezwa na wenda wazimu,
zinaleta ufahamu, na kubeza udhalimu,
Hizi ndo tungo tamu, ziburudivyo uoni.
Tungo tamu ni mwalimu, tungu ni mbovu dawamu,
Betize ni kama sumu, ijapo zatoka humu,
hufarikisha kaumu, insi wakamwaga damu,
Hizi ndo tungo tamu, ziburudivyo uoni.
Kumanya tungu na tamu,kwataka mwenye ilimu,
Wa kupembua magumu,ya guni pamwe nudhumu,
Beti hizi ni salamu, zifike hadi Kisumu,
Hizi ndo tungo tamu, ziburudivyo uoni.
Tamati tungu na tamu, ta'lamidhi na walimu,
Tungo hizi ni adimu, zaja kwenu kwa msimu,
Hima shikeni kalamu, kuyachukua magumu.
Hizi ndo tungo tamu, ziburudivyo uoni.
Wakatabahu.
Recent Posts
- Rashid Mkwinda03 Sep 2017NaViNjArI TaNzANiA- NILIPOTEMBELEA RAFIKI ZANGU WA KIMAASAI
Nipo na rafiki zangu jamii yaWamaasai tukibadilishana mawazo Nimetembelea rafiki zan...
- Rashid Mkwinda16 Aug 2017SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA LILIVYOTEKETEA KWA MOTO JANA USIKU
Eneo la Soko la SIDO jijini Mbeya lilivyokuwa likiteketea kwa moto jana usiku Sok...
- Rashid Mkwinda19 Jul 2017MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MKE WA DKT MWAKYEMBE KYELA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa Dkt Ha...
- Rashid Mkwinda18 Jul 2017MWILI WA MRS MWAKYEMBE WAWASILI MBEYA JIONI HII, MSAFARA KUELEKEA KYELA
Viongozi wa serikali wa mikoa ya Mbeya na Songwe mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mkuu wa mk...
- Rashid Mkwinda16 Jul 2017RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KIFO CHA MKE WA DKT. MWAKYEMBE
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...
- Rashid Mkwinda30 Jan 2017GOLIKIPA DAVID BURHANI AFARIKI DUNIA
Aliyewahi kuwa Golikipa wa kutegemewa wa timu za Majimaji ya Songea,Prison na Mbeya Ci...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ahsante, shairi limetulia kwa kituo.Na lugha unaitumia.
ReplyDelete