Ads (728x90)

Fasihi tunu adhimu, lugha njema kiswahili,
Watumiao adimu, toka zama za awali,
Hima enyi walimu,kuliangalia hili,
Lugha hii kiswahili, zawadi yetu adimu.

Taalamidhi Makene, sikiza ujumbe huno,
Na wengine waione, lugha isende pono,
Ingawa ipo karine, yaenda ja konokono,
Lugha hii kiswahili, zawadi yetu adimu.

Usuli wake sahili,ni nyepesi kutumia,
Yatokana na asili,Kibantu kino tulia,
Tutumie kihalali,lugha yetu kukuzia,
Lugha hii kiswahili, zawadi yetu adimu.

Shairi hili ni tunu,liangaze zote kona,
Ndesanjo acha ununu, jitokeze takuona,
Tutumie makala na mengineyo kiswahili kitakua.

Wakatabahu

Post a Comment