Ads (728x90)

Hebu leo niingie kivingine katika kuchangia kilichojiri,kwani mambo mengine yanaumiza sana moyo,taarifa zilizoripotiwa katika vyombo vya habari vya April 12 kutoka Mbeya vimenisononesha sana.
Eti mwanakijiji ameuawa kisa kutochangia ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata Sh 1500, na washiriki katiika kufanya unyama uliosababisha mauaji ya mwanakijiji huyo tunaambiwa kuwa ni Mwenyekiti wa kijiji hicho na Ofisa mtendaji wake wakishirikiana na Sungu sungu.
Imedaiwa kuwa Sungu sungu hao walimburuta mwanakijiji huyo katika ofisi ya kijiji na kumfunga kamba kisha kuanza kumpiga kwa mateke huku akichezewa sehemu zake za siri na kumuingiza mti katika tundu la haja kubwa huku Mwenyekiti na Mtendaji wake wakishangilia kitendo hicho, inatia uchungu sana eti kisa kukataa kuchangia Sh 1500 ya ujenzi wa shule ya Kata.
Kinachonifanya nijiulize zaidi hivi ni kweli ilikuwa sababu za mchango wa shule au walikuwa na ajenda nyingine? Haiwezekani kabisa watu wenye akili timamu tena wenye dhamana ya serikali kuchukua sheria mkononi ya kufanya unyama wa desturi hii.
Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi JK aliahidi kujenga shule katika kila Kata iwapo atapewa ridhaa ya kuongoza Taifa letu, tumempa ridhaa....ujenzi wenyewe wa shule katika Kata ni wa aina hii ya kuingizana miti katika njia ya haja kubwa na kuvutwa sehemu za siri?ni kweli Rais yupo radhi mpiga kura wake auawe kinyama kiasi hiki.
Ndio maana katika kuchangia hoja moja nilisema kuwa Kasi ya Kikwete imekuja bila kuwa na Fikra mpya iwapo kungekuwa na kasi mpya na fikra mpya matatizo kama haya ya watendaji kujichukulia sheria mkononi yasingetokea.
Kikwete asipoangalia atavurugiwa na watendaji wake kama hatabuni fikra mpya katika kasi mpya na nguvu mpya na ari mpya, jamani wanablogu hebu na tuchangie hili na kila mmoja aangalie uzito wa manyanyaso aina hii ya mwanakijiji aiyekuwa na hatia.

Wakatabahu

Post a Comment

  1. Mkwinda, habari ya kusikitisha sana hii. Uhai sio kitu cha kuchezea kama tambara. Lakini umemaliza kisa hiki kwa kusema jambo moja ambalo linanisaidia hata mimi kutazama vizuri zaidi hii serikali ya "ari mpya". Umesema kuwa hakuna FIKRA mpya. Nakuunga mkono. NChi imepelekwapelekwa kwa miaka mingi bila fikra za msingi za zinazoeleweka. Wakati wa Ujamaa, ingawa kulikuwa na makosa mengi, kulikuwa na fikra na pia visheni ya kueleweka.

    Swali ni: fikra mpya ni zipi?
    Asante kwa changamoto.

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mola Qudusi, muweke pema peponi ndugu yangu huyu aliyepotezewa maisha. Huwezi kuona hata kiongozi akifanya ziara ya ghafla katika tukio hili Mkwinda, tumegeuza nchi kuwa Dar es Salaam, na kuacha wakuu vijijini wageuke wafalme. Tumesihi katika manyanyaso ya aiba hii kwa miongo minne na ushee sasa.Huko Bush tufate nini bwana, kwani kuna video na umeme, kuna simu huko na kuna mabinti wanaojiupodoa? Kama unaweza na wewe uliye Mbeya tafuta Kitabu cha Mng'ng'o kiliichoitwa "Njozi iliyopotea" Naomba kumuoga mwenzangu na kukumbusha yule aliyefariki kwa kukosa shilingi 500 za matitabu Kagera, na wengine wengi ambao hawawezi kuandikwa wanaopatwa masaibu na kubaki kuchora ramani ya maumivu mioyoni mwao. Mola tazama mwanao.

    ReplyDelete
  3. Inasikisha sana hii. Mkwinda nisaidie jina la kijiji hiki.

    Nifafanue zaidi alilosema Makene maana anapunguza makali. Hivi majuzi Waziri Mkuu Ngoyai alitimka mbio kuelekea Chang'ome Village ambako matatizo ya kiufundi ya kagorofa (sio ya kibinadamu) yalisababisha kifo kimoja tu. Sasa tuone Mbeya kimetokea kifo cha mtu kilichosababishwa na watu wanaofahamika. Nani atatimka kwenda kuangalia huko. "Mbeya! Mbeya! Kuna nini Mbeya. Watusubiri mwaka 2010 watatuona"

    Watatuambia waziri wa ulinzi na usalama au RPC yupo Mbeya atamalizana na hili. Hivi Chang'ombe hakuna RPC au waziri mhusika wa ujenzi? Au ndio kasi ya magazeti maana ukionekana magazeti yanacopy ulilosema wedi-tu-wedi.

    ReplyDelete
  4. Bw.Mmwaipopo kijiji hicho kinaitwa Ntimba, Kata ya Msangano kipo wilaya ya Mbozi, ile wilaya ambayo hapo awali ilikuwa ni maarufu kwa biashara na uchunaji wa ngozi za binadamu,nadhani bado chembe chembe za unyama zipo kwa viongozi hawa wa kijiji,pia nina mashaka huenda ni miongoni mwa wachunaji wa ngozi za binadamu waliojificha chini ya kivuli cha Mwenyekiti wa kijiji na Ofisa mtendaji wa Kata, haiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu kufanya unyama kama huu.

    ReplyDelete
  5. Inasikitisha sana. Uhai usipothaminiwa namna hii.

    Swali: habari hii imesikika kwa walio wengi nyumbani? Kuna anayefuatilia?

    Nasikitika zaidi vile sioni nini cha kufanya kuhakikisha haki inatendwa.

    ReplyDelete
  6. Habari hii imenikumbusha filamu moja iliyochezwa na Danzel Washington, aliyoigiza mwanae anaumwa na hakuwa na namna yoyote ile ya kufanya ili kumponya maana uwezo hakuwa nao. Kwa walioiona filamu hii nadhani watakuwa wanaielewa uzuri. Ni mazingira ya namna hii hii.

    Pia inanikumbusha wakati fulani Bw. Kikwete, enzi hizo akiwa mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania, alipotangaza kaulimbiu yake ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya. Nakumbuka nilisema kuwa, kukimbia sio lazima iwe kwa kwenda mbele tu kama wengi tunavyodhania. Nilihoji wakati huo kuwa ni wangapi ambao wanajua kuwa kasi, ari na nguvu hiyo itakuwa ya uelekeo gani?

    Mungu amrehemu marehemu

    ReplyDelete