KISWAHILI ni miongoni mwa lugha zilizojichukulia sifa lukuki kwa makuzi yake katika nnnchi za Afrika mashariki, Afrika na ulimwengu kwa ujumla ambako kukua kwake kumechangia kwa upande mmoja ama mwingine kukuza maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Kutokana na kukua kwa lugha hii si aghalabu kuwasikia jamii ya watu wenye asili ya Kiafrika kuitangaza na kuitumia katika matumizi yao kama vile kwa njia ya usanii na vinginevyo.
Nimepata kumsikia msanii mmoja mwenye asili ya Kiafrika Michael Jackson akitumia vionjo vya lugha ya kiswahili katika moja ya nyimbo zake jambo linalotia moyo kwamba lugha hiii ikitangazwa kwa njia ya sanaa inaweza kuenea na kusambaa ulimwenguni kote.
Michael Jackson,mwanamuziki wa Kimarekani mwenye asili ya Kiafrika katika wimbo waake wa 'Liberian Girl' ametia vionjo vya 'Nakupenda pia!!nakutaka pia!! Mpenzi wee!!!'
Ajabu kwa wanamuziki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa hapa nchini ambao mara nyingi wanatumia nyimbo zao kwa mtindo wa fasihi simulizi, kwa kuigiza na kutunga tenzi na mashairi yasiyo na vina wala mizani sawia aambapo badala ya kutunga nyimbo zenye mantiki hutumia uwanja huo kwa kuimba nyimba ambazo hazina ujumbe wala kuifundisha jamii.
Utasikia mwanamuziki anaimba,''Twenzetu tukapige ulabu tukishakuwa Bwax tenzetu Klaabu tukacheki wachumba na mademu bomba''.
Maneno ylaiyomo katika ubeti huu wa moja ya nyimbo nyingi za wasanii wa muziki wa kizazi kipya hazifundishi lolote zaidi ya kuchochea ulevi na hamasa ya vitendo vya ngono ambapo hapo awali malenga na waimbaji wa zama hizo walitumia fursa yao katika nyimbo kuelimisha jamii.
Mie nadhani kuna haja ya hawa wasanii wa kizazi kipya kubadilika ili kwenda kwa mnasaba wa matakwa ya wadau wa lugha ya kiswahili ikiwa ni pamoja na kuchunga nidhamu ya lugha na muonekano wake kwa jamii.
Wakatabahu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment