Unakumbuka unyama huu enzi za utawala wa Bush nchini Iraq?
Angalia unyama huu na unyanyasaji dhidi ya raia walio nchini mwao, ni askari wa Marekani enzi za utawala wa Rais Bush mara walipovamia nchini Iraq na hapa ni mahabusu ambako raia wa Iraq walinyanyaswa na kuteswa kupita unyama hii ilikuwa May 4 2004.
Tazama askari hawa wa kimarekani walivyokuwa wamekithirisha unyama dhidi ya raia hawa wa Iraq, hivi kulikuwa na ajenda nyingine zaidi ambayo Bush alikuwa akiata kuifanya zaidi ya hii, kwanini hatua dhidi yake hazichukuliwi, mbona hafikishwi katika mahakama ya Kimataifa juu ya udhalilishaji huu alioufanya miaka ile?
Haivumiliki na tena haiyumkiniki kwa vitendo hivi kunyamaziwa kimya, hii ni changamoto kwa mrithi wa Bush,Rais Barack Obama ambaye nadhani atafuatilia kwa kina unyanyasaji huu uliokuwa ukifanywa na askari wa marekani dhidi ya raia wa Iraq.
BADO NASHANGAA KUONA JUMUIYA MBALI MBALI ZA KIMATAIFA ZIMEKAA KIMYA KUHUSU UTAWALA WA HUYU BUSH INAMAANA HAWAJUI ALIYO YATENDA AU WANAOGOPA KUSEMA WAKIOFIA WATAKOSA MISAADA AU SHERIA ZIPO KWAAJILI YA WANYONGE TU? INASIKITISHA SANA HII.
ReplyDelete