Ads (728x90)






Historia ya utawala wake iligubikwa utata ulioakisi imani yake ambayo ilikuwa ndani ya moyo wake hadi siku alipofariki dunia, hata hivyo hakuna hatua dhidi yake ambazo zilipatwa kuelezwa kuwa zinapaswa kuchukuliwa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa alifanya unyama wa hali ya juu kwa raia wasio na hatia wa nchi yake.Anaitwa Id Amin Dada aliyezaliwa 1925 katika mji wa Koboko Magharibi mwa Uganda na kutwaa madaraka kwa kuipindua serikali halali ya nchi hiyo ya Dkt. Milton Obote mwaka 1971 kabla naye hajang'olewa kutokana na vita vilivyomkimbiza nchi hiyo baina ya Uganda na Tanzania maarufu kama vita vya KAGERA, angalia picha picha ya hapo katikati jamaa huyu alikuwa ananyenyekewa na kusujudiwa na watu wa Mataifa ya kigeni na walimuogopa na kufyata mikia yao.picha ya pili kutoka ya juu ni Rais aliyepinduliwa na Id Amin mwaka 1971 Dkt.Apollo Milton Obote,picha nyingine ya juu kabisa ni Id Amin akiwa na wasaidizi wake ambao walikuwa wakimnyenyekea kupita maelezo.

Post a Comment

  1. Kwa haya mambo unayotukumbusha hapa ningependa kukuita mzee za zakale kwani wengi leo hii haya mambo tunajifunga mengi mengi sana

    Hongera tupo pamoja kamanda

    ReplyDelete