Ziwa lenye historia ya maajabu
Ziwa hili maarufu ambalo pia ni kivutio cha utalii lililopo kilomita kadhaa mashariki mwa wilaya ya Rungwe,linaelezwa na wenyeji wa eneo hilo kuwa lilizuka baada ya mtu mmoja kufika katika kijiji hicho na kuomba maji na baadaye kunyimwa na wenyeji wakazi wa hapo, ndipo mzee huyo aliyeonekana akiwa katika mavazi chakavu aliingia katika nyumba nyingine na kupewa maji, na kisha akamuamuru msamalia huyo aliyempa maji kuhama katika eneo hilo ndipo yalipozuka maji na kuzamisha familia ya mtu aliyemnyima maji mzee huyo mpita njia. Hata hivyo historia hiyo inapingana na maelezo ya baadhi ya wataalamu ambao wanadai kuwa chanzo cha ziwa hilo ni Volkano ambapo pia maji ya ziwa hiyo ni ya uvuguvugu hata kama kua baridi kali.
Duu kamanda umefika hadi huko huogpi hayo maji, maana nasikia ukiyagusa tu hayo maji nawe unakwenda na maji, hivi yana ladha gani ya chumvi au baridi
ReplyDelete