Ads (728x90)



Imekuwa ni desturi ya baadhi ya watu kutowajali watu wengine kutokana na hali zao kimaisha, iwe kiuchumi kimaumbile na hata kinasabu, wapo wanaowaona watu wengine ni bora kuliko wengine na kuwathamini baadhi yao na kuwadharau wengine,kwa kawaida Mungu amewaumba watu wote kwa kuweka tofauti baina yao akiwa na makusudi yake kwa wanaadamu, si vyema kumfanyia istihizai mmoja wenu kwa kuwa yuko katika hali fulani, heshima na utu ni jambo jema kwa kila kiumbe yoyote aliye chini ya jua awe Mlemavu kwa kiwango chochote cha ulemavu wake au Fukara kwa kiwango chochote cha ufukara wake kadhalika awe na Mkwasi kwa kiwango chochote cha Ukwasi wake, bali wote wanapaswa kuheshimiana na kuheshimiwa.Angalia picha hizi za mtu mmoja mwenye ulemavu, moja anapita katika ngazi ambayo kikawaida ni vigumu kupita kulingana na hali yake lakini picha nyingine anapita katika eneo lililojengwa rasmi kwa kupita watu wa aina yake,mazingira ya aina hii yapo kila sekta muhimu za kijamii, iwe mashuleni, maofisini hata katika maeneo mengine ya huduma ambayo watu wote bila kujali maumbile yao na hali zao wanapaswa kuhudumiwa huko.

Post a Comment