Hali si shwari nchini Misri Hosni Mubarak hataki kung'oka madarakani na wananchi hawamtaki tena askari wako upande wake nguvu ya wananchi inataka mabadiliko, ndiyo desturi ya viongozi wa Kiafrika kung'ang'ania walipo kwa njia yoyote ile hata ikibidi kumwaga damu, nini kipo nyuma yake kuna msukumo gani hapa,
Mfereji wa Suez,Uhusiano na Marekani,au utashi wa Israel? kwa nini Mubaraka na asiwe mwingine ameficha nini anaogopa nini kuachia ngazi,kama maji ya shingo si bora akimbile kwa hao wakubwa zake wanaomtaka aendelee kubaki?
Wamisri wenyewe wanataka mabadiliko hata kama italazimishwa Mubarak aendelee kuwa Raais ataongoza watu wa aina gani aamue kuachia ngazi hakuna tija kwa uongozi wa aina hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment