Hayati Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Waziri mkuu wa enzi hizo Hayati Rashid Mfaume Kawawa katika harakati mbalimbali za Uhuru wa nchi yetu.
Hayati Edward Moringe Sokoine atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kupingana na rushwa, ufisadi na hujuma dhidi ya mali za umma.
Jaji Joseph Sinde Warioba ni miongoni mwa watu wanaopaswa kuenziwa katika mchango wa nchi yetu kwa miaka 50 iliyopita.
Dkt. Salim Ahmed Salim, heshima yake inaendelea kutukuka ndani na nje ya nchi yetu, wananchi bado wanaheshimu fikra zake katika kupigania harakati za ukombozi na usuluhishi miongoni mwa nchi za Kiafrika.
Edward Lowasa Pamoja na kujiuzulu wadhifa wa Uwaziri mkuu kwa kipindi kifupi cha uongozi wa awamu ya nne anatajwa kuwa ni miongoni mwa viongozi mahiri walioamua kujitoa mhanga kwa ajili ya kulinda heshima ya serikali iliyopo madarakani na chama kinachotawala,Anaendelea kuandamwa kwa kashfa ya ufisadi kutokana na kitendo chake cha kujiuzulu wadhifa wa Uwaziri mkuu,huku tuhuma hizo zikimjengea heshima miongoni mwa wananchi na hata kuwa tishio ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Fredrick Sumaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa mawaziri walioitumikia nchi na kupiga hatua z amaendeleo kwa kipindi cha miaka mitano cha utawala wa awamu ya tatu ya uongozi wa nchi yetu.
John Malecela, mchango wake unaheshimiwa zaidi ndani ya chama na amekuwa miongoni mwa hazina zinazolindwa na chama tawala pamoja na kuwa nje ya uongozi na ulingo wa kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment