MJI wa Mombasa uliopo Pwani ya nchi
ya Kenya umekumbwa na machafuko na hali ya taharuki kwa waumini wa Kiislamu kufuatia kuuawa
kwa Sheikh Aboud Rogo ambaye awali alidaiwa kutuhumiwa kuhusishwa na kikundi
cha kigaidi cha El Shabab.
Kifo cha Sheikh Rogo ambaye ameuawa
mapema siku ya Jumatatu kimesababisha machafuko katika mji huo huku baadhi
ya watu wakielezwa kuingia katika vurugu
na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa.
Sheikh Rogo aliuawa kwa kupigwa
risasi akiwa ndani ya gari lake ambapo
siku kadhaa aliwahi kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za ugaidi, aliachiwa huru
baada ya kukosekana kwa ushahidi wa uhusika wake juu ya vitendo vya ugaidi,
mkewe wa mtuhumiwa huyo wa Ugaidi anaelezwa kujeruhiwa katika sakata hilo.
Mashuhuda wanaelezea tukio hilo kuwa
Sheikh Rogo alipigwa risasi akiwa katika mwendo kasi ndani ya gari lake.
Mwezi uliopitaa mahakama ya mjini
Nairobi ilimuamuru mkuu wa kituo cha Polisi cha Kamukunji kumchunguza Sheikh
Rogo na Sherif Abdullahi ambapo askari polisi waliwakamata wakiwa njiani
kuelekea mjini Nairobi.
Hayati Rogo na Sherrif walikuwa
wakisafiri kutokea mjini Mombasa kuelekea Nairobi ili kuhudhuria mahakamani
ambako walifunguliwa kesi juu ya tuhuma za vitendo vya ugaidi na mauaji.
Hayati Rogo amezikwa katika makaburi
ya Kikowani kwa mila na desturi zote za dini ya kiislamu.(chanzo thecitizen
Kenya)
Post a Comment