Na, Kibada
Kibada – Mpanda, Katavi.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda amewasili uwanja wa ndenge wa Kashaulili ulioko Mpanda Mjini Mkoa
wa Katavi kwa ajili ya mapumziko mafupi
.
Waziri Mkuu
Pinda mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mjini Mpanda alipokelewa
na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali Mkoani Katavi
kisha kuelekea kijijini kwake alipozaliwa Kata ya Kibaoni Kijiji cha
Kibaoni.
Akiwa
nyumbani kwake atapumzika na kusalimiana na wazazi wake pamoja na ndugu na
jamaa zake kijijini hapo.na mara baada ya
mapumziko hayo atafanya ziara ya kutembelea wapiga kura wake na wananchi
kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo mkoani
humo.
Mbali ya
kutembelea wananchi na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali
atakayopangiwa kwa mjibu wa ratiba pia atazindua bodi mpya ya barabara ya mkoa wa
katavi,pamoja na kufungua kikao cha kwanza cha ushauri cha mkoa mpya wa Katavi
, pamoja na shughuli nyingine za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzindua umeme
unaotumia nguvu ya jua maarufu kwa jina la umeme wa solar.
Baada ya
kumaliza ziara yake waziri mkuu atarejea
jijini Dar es salaam.
Katika hatua
nyingine mafunzo ya makarani watakaohusika na zoezi la sensa ya watu na makazi
yaliyokuwa yakifanyika maeneo mbalimbali mkoani katavi yamemalizika leo kwa
kufungwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima.
Akifunga
mafunzo hayo mkuu wa Wilaya ya mpanda
ameasaa makarani kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa ili kuweza kufanikisha
zoezi hilo muhimu la kuhesabu watu ili kupta takwimu sahihi kwa maendeleo ya
taifa.
Amesema
zoezi la sensa ni muhimu kwa taifa kupata takwimu sahimu ambazo zitasaidia
kutumika katika kupanga mipngo ya maendeleo ya taifa , shughuli za tafiti
na kupnga mipango ya sera ya kitaifa kwa
kuwa unakuwa na takwimu muhimu na hata kwa upande wa familia ukiwa na takwimu
sahihi zinasaidia kuweka mambo yako sawa sawa.
Kwa upande
wao wahitimu hao wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa umakini mkubwa kwa kuwa
kile walichofundishwa wamekielewa barabara ingawa kumekuwa na kasoro za hapa na
pale ambazo zinazungumzika na kurekebishika kuhakikisha zoezi la sensa
linafanikiwa vizuri.
Post a Comment