Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumie
Kisiwa
cha Ngkuyo kiko kilometa 11.1 kutoka bandari ya Mbamba_Bay. Kisiwa cha
Lundu kiko kilomita 13.6 kutoka hapohapo Mbamba_Bay.
Wakati pwani ya karibu kwa upande wa Malawi ni kwamba Ngkuyo kiko kilometa 45.9 na kile cha Lundu kiko kilomita 41.7.
Visiwa vyote hivi hasa Ngkuyo ni miliki ya Malawi enzi na enzi. Kisiwa hiki Ngkuyo ni maarufu kwa utalii na hujulikana kama Ngkuyo Island Rocks. Hiki Ngkuyo Island kinatangazwa sana duniani kama diving centre (Click here).
Ukitaka kuona zaidi watalii wanavyokaribishwa kuona aina ya samaki wa kisiwa hiki ambacho sehemu kubwa ni mawe angalia video hii.
Kwa nini nimeleta thread hii kwa suala lilelile la Malawi. Ni kweli ni suala lilelile lakini kwa context nyingine ili tupate kushirikiana kimawazo, ugumu ninaouona kila mara tunavyozidi kupekua suala hili.
Kwa kilomita nilizoweka hapo, kwa hali ya kawaida ni kwamba visiwa hivi viko kilomita chache sana kutoka pwani ya Tanzania kuliko pwani ya Malawi. Kilomita 11.1 za kutoka Ngkuyo Island ni sawa na jijini Mwanza kutoka Usagara kwenda Kigongo_Ferry.
Maana yake ni kwamba ukiwa Mbamba_Bay unakiona kisiwa hiki vizuri tu kwa macho. Lakini kutoka kisiwa hiki kwenda Malawi yaani kilomita 45.9 ni umbali wa kuzidi Mwanza hadi Ukerewe kwani kutoka Kayenze hadi Nansio pale Ukerewe ni kilomita 30.5 tu.
Sasa, tunapofikiri kwamba tunaweza kupata mpaka ukawa nusu kwa nusu, basi maana yake Malawi iache kabisa kuvitumia visiwa hivi kwa shughuli yoyote bila ruhusa yetu hata kama tangu kuja kwa wakoloni walivitumia kama vya Malawi na dunia nzima ikafahamu hivyo!
Je, watakubali kiasi hicho. Ndiyo tuone ugumu wa suala hili. Ugumu ambao kitabu hiki kilishauzungumza kwenye ukurasa wa 249 {Click here}.
Ukisoma hapo utaona kwamba mimi nimetaja visiwa hivi viwili lakini yeye kavitaja vitatu yaani Ngkuyo, Lundu na Papia.
Binafsi, hapa ndipo nadhani hata mawaziri wote wameshaeleza kwamba suala hili ni gumu na inaweza likafikisha International Coast of Justice.
Visiwa ni sehemu muhimu sana. Kisiwa cha Bongoyo kiko kilometa 5.2 kutoka Msasani_slipway. Kisiwa cha Saa Nane hakizidi kilomita mbili kutoka Tilapia Hotel pale Mwanza.
Lakini leo useme unachukua kisiwa cha Bongoyo au ufanye lolote kwa kisiwa cha Saa Nane hakika hapo unakaribisha mengine tu.
Ndiyo na wamalawi wanavyoviona visiwa hivi ambavyo havijawahi kuwa vya nchi nyingine japo tumeona kwamba viko jirani zaidi na Tanzania. Lakini tunaposema mpaka uwe nusu kwa nusu basi fikiri mara mbili maana kuna baadhi humu walidhani ni maji tu hakuna masuala kama haya.
Na kama ndege zilizotua majini zilifukuzwa sasa sijui kwa nini matumizi ya utalii kwa visiwa hivi hayakukatazwa tangu kale? Je, kama kweli ndege zilizuiwa je, visiwa hivi vimehamishwa visiwe karibu na Tanzania. hapana haiwezekani. Je, shughuli za utalii za Malawi zimesimamishwa? Binafsi sijasikia labda nyinyi wenzangu.
Kama ni hivyo, basi nina haki ya kusema na sisiti kusema kukataza ndege zisitue majini ni sawa kabisa na kusema shughuli yoyote ya ziwani mle maadamu iko kwenye ile nusu inayoelekea Tanzania isiendelee.
Hivyo, sisiti kusema kusimamisha utafiti wa zile ndege kwenye nusu hii na kuacha shughuli za utalii ni unafiki usioweza kutetewa kwa njia yoyote.
Ukweli ni kwamba shughuli za utalii na kila kitu kwa visiwa hivyo zinaendelea. Tuachane na hayo turudi kwenye kujiuliza. Kama tutabahatika kushinda na nusu ikawa kwetu, je umiliki wa visiwa hivi utakuwaje?
Ni rahisi sana kukurupuka na kusema vitakuwa vyetu. Si rahisi kiasi hicho. Hapa ndipo inabidi tuangalie nini kilitokea kwenye ziwa hilohilo kwa upande wa Mozambique. Ukweli ni kwamba mpango mzima wa kwanza ilikuwa ziwa lile mipaka ipite ukingo wa mashariki kama ilivyofanyika Tanzania. Lakini Portugal ikaingia mkataba walau kupata sehemu ya ziwa hilo.
Mkataba ulipoingia Nyasaland wakapewa milima kadhaa na Mozambique ikapewa portion ya Ziwa na ndiyo sababu kuna sehemu kule mpaka wa Mozambique unaingia ziwani.
Lakini badi hiyo haikutosha. Wakati wanagawa hivi, ikaja kesi ya visiwa kadhaa kikiwemo kisiwa cha Lukoma. Ile nusu waliyopewa Mozambique ikawa inakimeza kisiwa hiki Lukoma. Lakini makubaliano yale ya Portugal na Britain yaliweka wazi kwamba Lukoma Island kweli iingie ndani ya Mozambique territory lakini ibaki kwenye ownership ya Nyasaland!
Hivyo, ukiiangalia Lukoma kwenye ramani unaweza kukurupuka na kusema ni sehemu ya Mozambique. Na wala si kukurupuka tu, kama huijui histiry hii kama wengi wasivyijua kuhusu mipaka hii na wakawa hawajaka notekey yoyote basi hakika utasema Lukoma ni sehemu ya Mozambique wakati ukweli ni sehemu ya Malawi.
Hali hii ya Lukoma yaani eneo fulani la Malawi kuwa ndani ya eneo la nchi nyingine huitwa exclave. Ni tofauti na Britani kuwa na Falkland au USA kuwa na Alaska na Hawaii kwa sababu hayo hayajazunukwa na nchi nyingine.
Hivyo, tunapojadili hili suala la Malawi, tu-explore possibilities zote ambazo tunaweza kuziona ngeni na tukaishia kupiga kelele kwa sababu tu ya kutokujua.
Binafsi, bado sijawa na hakika kama tutapata ziwa hili kama tunavyolihitaji. Lakini tukilipata basi tusisahau kwamba kesi ys Lukoma kule Mozambique inaweza kuwa imeweka precedent kiasi kwamba visiwa hivi tunaweza tusivipate hata kama tunaweza kupata nusu ya ziwa.(chanzo jamiiforums)

Post a Comment