Ads (728x90) 
Kikosi cha Mbeya City ambacho kabla ya mechi yake na Ndanda ilikuwa inaongoza kutoka mwisho ikiwa na alama 5.

Ndanda FC ambao walikuwa wanashikilia nafasi ya pili kutoka mwisho waliopoteza mchezo wake na Mbeya City kwa kufungwa Bao 1-0.

Mechi inaendelea
 
Patashika Uwanjani

Hatari!!! katika goli la Ndanda FC

KUTOKA KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE JIJINI MBEYA NI MIMI RASHID MKWINDA WA FASIHI MEDIA INC.

TIMU ya Mbeya City ya Jijini hapa imejinasua kutoka mkiani baada ya kuifunga timu ngeni katika Ligi kuu ya Vodacom kwa Bao 1-0.
Mbeya City ambayo msimu uliopita ilikuwa tishio kwa timu kubwa baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga za Jijini Dar es salaam ilianza kuwakatisha tamaa mashabiki wake kwa kupoteza michezo mingi ya ligi hii.
Hadi inaingia katika mchezo wa leo Mbeya City ilikuwa inaongoza kutoka mwisho huku ikiwa ina akiba ya pointi 5, baada ya ushindi wa leo imejikusanyia jumla ya alama 8.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikiwa na uchu wa kupata goli ambapo ilikuwa katika dakika ya nne ya mchezo, Mbeya City ilijipatia goli lililofungwa kwa njia ya kichwa kupitia kwa mchezaji Deus Kaseke.
Kaseke alifunga bao hilo baada ya pasi kutoka kwa Themi Felix aliyeupokea mpira kutoka kwa Paul Nonga.
Golikipa wa Ndanda alichupa bila mafanikio na mpira ulitinga wavuni.
Hadi mapumziko Mbeya City ambayo ilikuwa inashangiliwa na mashabiki wachache tofauti na ilivyokuwa katika mechi zilizopita za ligi hiyo ilikuwa kifua mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Mbeya City ilimuingiza Mwagane Yeya badala ya Cosmas Fredy na  Ndanda walimuingiza Said Issa badala ya Nassoro Kapama na Idd Kulachi aliyeingia badala ya Masoud Chile.
Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda wala kubadilisha matokeo ya mchezo huo ingawa kwa upande wa Ndanda United kulionesha kuwa na uhai katika safu ya ushambuliaji.
Ndanda walicheza kwa kasi katika kipindi cha pili na kuudhibiti mpira kwa muda mrefu huku Mbeya City wakionekana kupoteza muda kwa kuanguka anguka mara kwa mara.
Hadi kipyenga cha mwamuzi wa kike Mary Kapinga kutoka mkoani Ruvuma kinapulizwa Mbeya City imetoka kifua mbele kwa goli 1 dhidi 0 ya Ndanda United.
Hata hivyo kocha wa timu ya Ndanda FC Meja Mstaafu Abdul Omar alisema kuwa goli walilofungwa halikuwa halali kwa kuwa wachezaji wa Mbeya City walikuwa wameotea.
Alisema kuwa wachezaji wake walicheza kwa kujituma ingawa uwanja ulikuwa ni tatizo kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Jijini humo kabla ya mchezo huo.
Naye Kocha Juma Mwambusi alisema kuwa ushindi wa timu hiyo ulitarajiwa kutokana na jinsi walivyojipanga katika mechi zilizopo na kuwa makosa yaliyotokea katika michezo ya awali yamerekebishwa.

Post a Comment