Ads (728x90)

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadharani mjini Tukuyu wilayani Rungwe jana.

Mamia ya wakazi wa mjini Tukuyu wakimuunga mkono Mwenyekiti wa CHADEMA kutosogeza mbele uandikishwaji wa wapiga kura ulianza kuendeshwa kwenye baadhi ya mikoa nchini

Baadhi ya wakazi wa Ushirika Kata ya Mpuguso wilayani Rungwe wakiwa wamelala barabarani kumsubiri Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu akihutubia mkutano kabla ya kumkaribisha Mbowe katika viwanja wa Tukuyu wilayani Rungwe jana.



Mbowe akishuhudia uandikishwaji wa wapiga kura katika kituo cha Mpuguso wilayani Rungwe.

Mmoja wa wazee wa kijiji cha Mpuguso akiwa amelala chini kuonesha ishara ya upendo na utiifu mbele ya Mwenyekiti wa  CHADEMA Freeman Mbowe.

Hii ni kauli ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo “CHADEMA”Freeman Mbowe aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji wa Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya, juzi jioni.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro aliyasema hayo kwa niaba ya viongozi wa Muungano wa UKAWA akiwataka wananchi wa wilayani Rungwe kujitokeza kujiandikisha katika daftari la Wapiga kura ambalo pia alisema limegubikwa na dosari nyingi.
Alisema kuwa ana uhakika mkubwa wa UKAWA kuiong’oa CCM madarakani Oktoba mwaka huu na kuwataka viongozi waliopo madarakani kutubu kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwadhulumu Watanzania na kuwa katu wao hawatalipiza kisasi kwa matendo yao kwa Watanzania.
‘’Hii si nchi ya kulipizana kisasi bali tunapaswa kuangalia mambo ya msingi ya kutujenga sote badala ya kupoteza muda wa kulipiza kisasi kwa makosa ya wachache,’’alisisitiza Mbowe.
Alidai kuwa kuna kila dalili za hujuma dhidi ya uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu kwa kuwa zoezi limefanywa kwa kupoteza muda bila sababu za msingi jambo ambalo lilipaswa kufanywa kila baada ya miaka mine.
Alisema kwa kipindi cha zaidi ya miaka saba hakukuwa na mchakato wowote wa uboreshaji wa daftari hilo na kutegea zikiwa zimebaki siku chache ili kuwe na sababu za kusogeza mbele uchaguzi mkuu jambo ambalo UKAWA hawako tayari kukubali.
‘’Hatutokubali kusogezwa mbele uchaguzi mkuu hata kwa siku moja, tunaomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye iwezavyo ili asiwepo mwananchi mwenye haki ya kujiandikisha akakosa fursa hiyo’’alisema.
Aidha Mbowe aliwaasa watia nia wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kugombea nafasi zao kwa nia ya kweli badala ya kutanguliza ubinafsi na kuwa chama hicho hakitawapokea wagombea wanaotanguliza maslahi binafsi.
Alisema viongozi waliotia nia wanapaswa kufuata Katiba ya chama hicho na kwamba yeyote atakayekiuka katiba hatovumiliwa na chama hicho kwa kuwa kinajengwa wenye nia thabiti ya kuwatumikia Watanzania.
Alibainisha kuwa chama hicho hakina ubinafsi kama ilivyoenezwa propaganda dhidi yake na kuwa kama kungekuwa na ubinafsi yeye Mbowe angekuwa mtu wa kwanza kukihodhi chama hicho kwa kuwa ametumia fedha zake za mfukoni kukifikisha hapo kwa zaidi ya miaka 20.
‘’Kama kungekuwa na ubinafsi mimi Mbowe ningesema chama hiki ni mali yangu, nimetumia rasilimali fedha zangu kutoka mfukoni mwangu na kukifikisha hapa kilipo,’’alisema na kuongeza.
‘’CHADEMA ni sawa na treni ambayo abiria wake ni wavumilivu,wako wanaokosa uvumilivu ambao hushukia njiani hawa ni wale wanaokiuka Katiba ya chama chetu,’’alisema.
Mbowe ambaye aliambatana na wabunge wanne wa chama hicho Joseph Mbilinyi(Mbeya mjini) Rebeka Mngondo (Viti maalumu Arusha)Cesilia Pareso(Arumeru) na Naomi Kaihula (Viti maalum Mbeya) wamefanya ziara mkoani Mbeya na kutembelea wilaya za Rungwe na Kyela ambako zoezi la uandikishaji wapiga kura linaendelea.

Post a Comment