Ads (728x90)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa Dkt Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe leo mchana nyumbani kwa marehemu kijiji cha Ikolo wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa na shada la Maua kwa ajili ya kuweka katika kaburi la mke wa Dkt Harrison Mwakyembe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha Maombolezo ya mke wa Dkt Harrison Mwakyembe
Waziri mstaafu  katika serikali za awamu ya Tatu na ya  Nne Prof Mark Mwandosya akielezea masikitiko yake juu ya kifo cha mke wa Dkt Mwakyembe
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Job Ndugaai akisalimiana na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu)walipokutana kwenye msiba wa mke wa Dkt Harrison Mwakyembe leo mchana.

Mkuu wa mkoa Mstaafu wa mkoa wa Kilimanjaro Cynthia Ngoye na Mkuu wa mkoa mstaafu Mbwilo wakiwa na shada la maua kwa ajili ya kuweka kwenye kaburi la mke wa Dkt Mwakyembe.
Mke wa Spika wa Bunge mstaafu marehemu John Samwel Sitta, Margrethy Sitta akibubujikwa na machozi,huku akisindikizwa na mwanaye wakati wa mazishi ya mke wa Dkt Mwakyembe.
Mbunge wa Jimbo la Songwe Philipo Mulugo akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa mazishi ya mke wa Dkt.Mwakyembe

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi Sugu alipata fursa ya kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya CHADEMA.

Watoto wa marehemu Linah Mwakyembe wakiwa na shada la maua kwa ajili ya kuweka juu ya kaburi la mama yao

Waziri mkuu mstaafu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye akiweka shada la maua juu ya kaburi la mke wa Dkt Mwakyembe.

Waziri Mkuu mstaafu mzee Samwel Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango walihudhuria mazishi ya mke wa Dkt Mwakyembe.

Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mke wa Dkt Mwakyembe.

Post a Comment