Ads (728x90)

Naam ni mwaka mmoja wa Mheshimiwa JK, nini mustakabali wa SIHASA hapa nchini kwetu, ndio mwanzo wa kuua vyama vya upinzani au ndio chachu ya kuimarisha demokrasia?lakini ni vigumu kupima maendeleo ya nchi kwa siku 365-1/4 bali la muhimu kuangalia utekelezaji wake jee una manufaa kwa wananchi au ndo nyimbo hizo za kila siku za maisha bora kwa kila Mtanzania?.

Juzi nilikuwa katika kijiwe cha kahawa mahala fulani, kile nilichokisikia katika kijiwe kile kilinitia mshawasha wa kupandisha komenti hizi, katika kijiwe hicho nilisikia vijana wakishabikia Sh. Bilion 21 za serikali zilizotolewa kwa kila mkoa.

Nilimsikia kila mmoja akipanga bajeti na majukumu yake, mara baada ya kupata fedha hizo, kilichonishangaza na haswa kupata hamu ya kutoa fikra zangu ni baada ya kutafakari na kuona kuwa fedha hizo si lolote wala chochote,baada ya kutokea jamaa mmoja ambaye alianza kuzipigia hesabu fedha hizo kulingana na takwimu ya wahitaji.

Jamaa huyo alinipigia Sh. Bilion 21 ambazo ni sawa na Sh. Milion 1000 kwa kila mkoa ambao unatarajiwa kupata Sh. Milion 1, ambapo pia akapigia wastani wa wilaya tano na kupata kila wilaya inaweza kupata wastani wa Sh.Milion 200 ambapo pia akapigia kwa wastani wa kata 10 na kupata wastani wa kila kata moja kupata Sh. laki 5.

Kadhalika katika mahesabu yake alipigia wastani wa vijana 1000 kwa kila kata wakawa ni wahitaji wa fdha hizo akagawanya kwa laki tano akapata kiasi cha Sh.elfu tano kwa kila kijana pia akajaribu kuangalia bei ya mbolea kabla hajatolewa ruzuku ya serikali ya mfuko Sh.35,000, hapo ndipo nilipoachama mdomo na kusema kuwa huu ni usanii.

Nikajiuliza swali moja hivui serikali imefanya upembuzi wa kina kujua kama ni kweli hizo Milion 21 zinaweza kukiddhi mahitaji ya walalahoi na hivyo kuwa na maisha bora kwa kila Mtanzania nikagundua kuwa kuna usanii ulio wazi ambao kwa hakika mtu wa kawaida hawezi kubaini.

Ndugu zangu hii nchi ni yetu na sisi sote ni wahitaji wa kile kilichomo ndani ya nchi yetu, hivi ni kwa nini basi tuwe tunadanganywa kama watoto wadogo, tuangalie uhalisi wa maisha ya mwananchi wa kawadia ambaye aghalabu huambulia mlo mmoja kila siku na kutafakari namna ya kupata mlo kwa siku nyingine.

Maisha ya mtu wa aina hii ambaye elimu yake, afya yake, malazi yake pamoja na huduma za matibabu zinahitaji fedha anaweza kujikimu na kuishi katika anga hili na akajivunia kuwa yuko katika maisha bora?

Hili ni swali ambalo ninajiuliza binafsi na kila mmoja anaweza kuwa na wazo lake binafsi, na tuangalie kama ni kweli tuko katika mapambano ya umaskini kuelekea sera kuelekea 2025 kama inavyoeleza sera ya Taifa ya kukuza uchumi na kuondosha umaskini MKUKUTA.

Wakatabahu

Post a Comment

  1. Ukibaki kwenye hizo tarakimu (bilioni sijui ngapi) unaweza kuona ni fedha nyingi sana, ila ukiingilia mahesabu hayo uliyotoa unagundua kumbe ni usanii.

    Kwanza ni lini tumekuwa na utaratibu wa kusimamia masuala ya fedha nchini? Fedha zinatolewa kila siku kwenda kwenye miradi mbalimbali lakini hazifiki kunakotakiwa. Bila utaratibu wa wazi na unaojaribu kwa kila mbinu kuzuia au kupunguza ufujaji, bado tutakuwa kwenye hadithi ambayo imezoeleka nchini.

    ReplyDelete
  2. Hapana. Hizo tarakimu hata kwa maelezo gani si sahihi. Huu mtindo wa wahasibu kuongeza sifuri katika tarakimu zilizoko ndio sababu.

    Fedha katika nchi hii inaonekana hazina mwenyewe. Kila mtu anamega apendavyo.

    ReplyDelete