Ads (728x90)



Hebu jaribu kulinganisha maisha haya na yale ya mwaka 1970 kama ulikuwepo chini ya jua hili kule kijijini kwako, yana tofauti gani?kwa taarifa yako akina mama hawa ndio mtindo wao wa kujipatia riziki kila siku iendayo kwa Mungu, hufuata mizigo hiyo ya kuni umbali wa km 15 na kuzileta mjini kisha huuza kwa mzigo mmoja sh.1000,na mara nyingi kuni hizo huuzwa kwa siku mbili au tatu labda apatikane mteja wa haraka, hata hivyo huko wanakozifuata hukumbana na misukosuko ya kufukuzwa na mabwana miti, hapo walipo wana watoto wanawasomesha, na wanahitaji kupata chakula kila siku, achilia mbali sukari kwa ajili ya chai asubuhi hiyo wamesahau kabisaaa, watoto wakiamka asubuhi hufunua masufuria na kuangalia kama kuna kiporo cha ugali na maharage kilibaki jana usiku kama hakuna ndio ntoleee!!! hadi jioni kama mama amefanikiwa kuuza mzigo wa kuni na kununua kibaba cha unga.Usishangae sana hayo ndio maisha ambayo jamii yetu tumeyazoea na tunaendelea kuishi miaka imakatika, huku wanasiasa wakitufuata wakati wa kampeni na kutudanganya kwa kilo moja moja za sukari, khanga, kofia na tsheti, tunapokea na kuwapa kura sasa unadhani tutafanyaje? mie nawapa tu kura atakayenilaumu na wacha anilaumu mbona nimezoea haya maisha!!!!!

Post a Comment