Ads (728x90)


Rais wa sasa wa Malawi Bw. Bingu wa Mutharika ambaye ni rais wa tatu ambaye naye alimshinda Alhaji Muluzi katika uchaguzi wa kidemokrasia chini ya mfumo vyama vingi.

Pichani Alhaj Bakili Muluzi aliyechukua nafasi ya Dkt.Kamuzu Banda mwaka 1994 mara baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini humo mwaka 1992.

Ngwazi Dkt. Hastings Kamuzu Banda kiongozi na mwanasiasa wa Kiafrika na Rais wa Malawi kati ya mwaka 1966 hadi mwaka 1994 ni mtoto wa mkulima aliyetunukiwa shahada ya udaktari nchini Marekani ambapo baada ya vita kuu ya pili alifanya kazi ya udaktari London nchini Uingereza na hapo ndipo ilipoanzia chachu ya uongozi wake alirejea Afrika mwaka 1953 na baadaye nchini mwake Malawi wakati huo ikijulikana kwa jina la Nyasaland mwaka 1958 na kufanya kampeni juu ya shirikisho la Nyasaland dhidi ya Rhodesia(Sasa Zimbabwe na Zambia).

Hadi kifo chake mwaka 1997 Rais huyo aliyetawala nchi hiyo kwa takribani miaka 23 kati ya mwaka 1966 hadi mwaka 1994 hakufahamika vizuri mwaka aliozaliwa ingawa kulikuwa na hisia kuwa huenda alizaliwa kati ya mwaka 1896 na mwaka 1906 na hivyo kumfanya aishi kwa kati ya miaka 95 au 98 hadi kifo chake.Amezaliwa karibu na mji mdogo wa Kasungu nchini Malawi.

Mwaka 1961 Dkt. Banda chini ya chama chake cha Malawi Congress Party(MCP) alishinda uchaguzi nchini humo.

(NGWAZI DKT.HASTINGS KAMUZU BANDA ENZI ZA UJANA WAKE)
Dkt. Banda na Nyasaland akiwa ameshikilia wadhifa wa Waziri mkuu akaifanya nchi yake kupata Uhuru mwaka 1964 chini ya mfumo mpya hatimaye mwaka 1966 akawa Rais wa Malawi na baadaye mwaka 1971 alijitangaza mwenyewe kuwa ni Rais wa Maisha wa nchi hiyo 'President wa Muyaya' na ni mwaka huo huo alikuwa ni rais wa kwanza wa nchi za Afrika kutembelea nchini Afrika kusini enzi zile za utawala wa kibaguzi, wakati ambao baadhi ya watu wakiuawa na wengine kufungwa nchini Afrika kusini Rais Banda aliishi kwa raha mustarehe nchini Afrika ya Kusini. Hali hiyo ilifanya baadhi ya nchi za kiafrika kumtuhumu kwamba alikuwa akitumiwa na nchi za magharibi.

Wimbi la mageuzi kutoka nchi za magharibi lilipoingia katika nchi za Afrika mwaka 1992, liliathiri fikra za Rais Banda na kulazimika kuingia katika mfumo wa vyama vingi kutoka mfumo wa chama kimoja na kuvunja hisia zake za kuwa rais wa maisha wa nchi hiyo mwaka 1993 ambapo katika uchaguzi wa kidemokrasia na mfumo wa vyama vingi mwaka 1994 mshindani wake Bakili Muluzi alishika uongozi wa nchi hiyo aliyeshika uongozi wa ncji hiyo hadi mwaka 1995.

Post a Comment